Na Mwandishi wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Jakaya Kikwete, atalihutubia bunge maalum la katika Ijumaa ya Machi 21 saa
10:00 jioni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa
bunge maalum, hotuba ya Rais Kikwete ndio itakayoashiria wajumbe kuanza kazi ya
kuijadili rasimu.
Taarifa hiyo imesema uteuzi wa wajumbe wa Kamati
za bunge maalum utafanyika Ijumaa asubihi.
Semina kuhusu rasimu ya katiba itafanyika kesho
ikitanaguliwa na semina kuhusu kuzifahamu kanuni inayofanyika leo.
Kuhusu wajumbe ambao bado hawajaapishwa taarifa
hiyo imewataka kufika Idara ya shughuli za bunge maalum kwa ajili ya kutambuliwa.
Naomba nijulishe kuwa Rais atalihutubia bunge la katiba March sio January kama ilivoripotiwa hapo,
ReplyDeleteNaomba kuwakilisha
anaenda kuhutubia au kutisha wabunge wafanye vile anavyotaka yeye? kama alivyofanya nyerere wakati ule akamlazimisha aboud jumbe kujiuzulu, nawaomba wajumbe waznz wawe kitu kimoja hakuna kuogopana , wa kuogopwa ni mwenyezi mungu pekee , yeye na aje aseme anachotaka , sisi uhuru wa zanzibar upo pale pale , muungano hatuutaki kabisa , wala serikali tatu hatuna haja nazo wabakie nazo wenyewe watuachie visiwa vyetu basiiii tenaaaa
ReplyDelete