KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo na Misitu Ndg. Affan Othman Maalim, akitiliana Saini na Mtaalam wa Kilimo cha Umwagiliji Maji kutoka Korea,Ndg. Yoon Chang-Jin, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Darajani.
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo na Misitu Ndg. Affan Othman Maalim akibadilishana mkataba baada ya kutiliana saini na Mtaalam kutoka Korea. Ndg. Yoon Chang-Jin, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Darajani.(Picha na Juma Aboud Talib - Kilimo)
Na Khamisuu Abdallah
WIZARA ya Kilimo na Maliasili Zanzibar imetiliana
saini na serikali ya Jamhuri ya Korea
Kusini kutekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ili
kuimarisha uzalishaji wa mpunga nchini.
Jumla ya dola za Marekani milioni 50 zinatarajiwa
kutumika katika mradi huo ambazo ni mkopo kutoka benki ya Exim ya China .
Hafla ya utiaji saini huo imefanyika jana katika
ukumbi wa Ofisi ya Wizara hiyo Darajani, ambapo kwa upande wa SMZ imewakilishwa
na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Affan Othman Maalim.
Akizungumza baada ya utiaji saini, mtaalamu kutoka
shirika la Korea Rural Community, Dk. Yoon Chang- Jin, alisema lengo la mdari
huo ni kuongeza uzalishaji wa chakula na hasa mchele na kupunguza uagizaji
kutoka nje.
Alisema
uzoefu wa nchi ya Korea
utaweza kuisadia Zanzibar katika sekta ya kilimo hasa
miundombinu ya umwagiliaji ili iweze kuinua kilimo cha mpunga na kujitegemea
kwa chakula.
Aidha mtaalamu huyo alisema mradi huo utatekelezwa
kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ni kupima na kuchora mabonde yote ya
umwagiliaji na awamu ya pili ni kuwapelekea wakandarasi kwa ajili ya ujenzi miundombinu ya kusambazia
maji.
Alisema wameridhishwa na utafiti uliofanywa na
Wizara hiyo na kuahidi kushirikiana katika uwekaji wa mazingira mazuri ya
kilimo.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili,
Affan Othman Maalim, alisema mpango huo utakapokamilika jumla ya hekta 2,200
zinatarajiwa kuingizwa kwenye mdari huo.
Aliyataja mabonde yatakayofaidika kuwa ni pamoja na
Cheju, Chaani, Kibokwa na Kilombero kwa Unguja na kwa Pemba
ni Mlemele na Makwararani.
Aidha Katibu huyo alisema mradi huo ukikamilika
asilimia 50-70 ya mchele utakuwa unazalishwa Zanzibar .
mhhh hizo hesabu sijui kama mnafanya vizuri au vipi , milioni 50 dolla ni sawa na bilioni 80 za tanzania kila siku huwa tunasikia kilimo cha mpunga ambcho kitatatua tatizo la mchele kwa asilimia 50-70 , kweli kujitia deni kama hilo kuna umuhimu wowote? sisi tuna mvua nyingi tu nchini kwetu sisemi umwagiliaji usifanyike lakini hio fedha kutoka kwa mgongo wa mlipa kodi ni nyingi , nyinyi viongozi wetu pengine mshatia pasenti humo hamjali na wengi mtakuwa mshakufa wakati sisi tunaendelea kulipa deni , hapa kuna walakini , tena ndugu katibu nakuona una upo kwenye kila sunna hapo ulipo jee umeangalia hili jambo kwa uadilifu kama vile kivazi chako kinavyoonyesha? una sijida mwenzetu sisi wengine hatuna chochote, mimi sijasoma kama wewe lakini kwa hesabu ya haraka haraka haingii kichwani kutia nchi deni kubwa wakati hakuna tatizo la mchele znz, unatoka nje unatutosha huo unaolimwa hapo ungeendelezwa kwa namna nyengine lakini sio deni kama hili wakati bado tutabakia kuagiza nje , na kwa kawaida huu mchele unaagizwa na wafanya biashara binafsi , sioni kwa nini serikali itumie fedha nyingi kwa kutatua tatizo ambalo halipo
ReplyDelete