Na Hanifa Salim PEMBA
JUMLA ya wanafunzi 1,222 na walimu 13 katika skuli
ya Kangagani msingi na sekondari mkoa wa kaskazini Pemba, wamefaidika na mradi wa maji ulitolewa na
Jumuiya ya Zanzibar
Outreach Program (ZOP) kwa lengo la kudumisha afya zao.
Mradi huo, uliozinduliwa rasmi Machi 5 mwaka
huu katika skuli hiyo umegharimu shilingi milioni 4.5 ni kwa ajili ya wanafunzi
na walimu wa skuli hiyo.
Mwalimu mkuu wa skuli ya sekondari Kangagani,
Hasina Ali Makame, alitoa shukurani zake za dhati kwa ZOP kwa kuondoa
changamoto iliyokuwa ikiwakabili kwa muda mrefu.
Kwa upande wake, Katibu wa ZOP, Dk. Nofal
Kassim Mohamed, aliwataka walimu na wanafunzi wa skuli hiyo kutumia vizuri
mradi huo ili udumu kwa muda mrefu.
Alisema anatarajia mradi huo utaondoa tatizo la
uhaba wa maji lililokuwa likiwakabili wanafunzi na walimu hali iliyosababisha
kwenda nyumba za jirani kuomba maji.
Nae, daktari wa meno kituo cha afya Micheweni,
Abeid Zubeir Khamis, alisema ZOP wataendelea kuimarisha huduma za afya hasa kwa
wananchi wa vijijini.

No comments:
Post a Comment