WANANCHI
na wafanyabiashara wa mji wa Wete Pemba,
sasa wako katika furaha, baada ya shirika la bandari la Zanzibar, kuimarisha
gati kwenye bandari ya mji huo, pichani makuli wakipakua mizigo kwenye mashua
zinazosafiri baina ya mji wa Wete na Tanga (picha na Haji Nassor, Pemba)
WAZIRI MKUU: SERIKALI YATENGA 43BN/- KUIMARISHA MICHEZO SHULENI * Azindua
mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA Iringa
-
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kwenye uzinduzi wa Mashindano ya
UMITASHUMTA na UMISETA kwa Mwaka 2025, ambayo yatafanyika Kitaifa Mkoani
Iringa...
43 minutes ago
Subhaanallah,huko ndio kuimarika?
ReplyDeleteAssalaam alaykum ndugu wapendwa na wanzanzibari wenzangu. Kwa kweli nimeshangazwa na hii habari pamoja na picha.Hii gati ndio imeimarishwa hii, hivi najiuliza hapo kabla ilikuwaje, mimi sioni jipya wa kubwa. Jamani viongozi wetu tuache kufanya dhihaka na wananchi wanyonge wa nchi hii, tusitumie unyonge na idhaifu wetu kutukandamiza jamaniiiii eeeeh. Viongozi Tumuogope allah. Hivi kisiwa hiki cha Pemba kwa miaka yote hii kimekuwa ndio mchangiaji mkuu wa pato la Taifa kwa asilimia zaidi ya 80% kwa kuzalisha karafuu (Kabla ya kuja huu utalii), hivi inaelekea kuwa na gati /bandari kama hii kwa miaka yote hiyooo. Heee jamani viongozi wetu tujuwe kwamba nyinyi ni mas-uul mbele ya allal na muelewe kwamba mutaulizwa vipi mumewaongoza wananchi wenu pamoja na kuwafikishia huduma na haki zao mbalimbali, tusilewe madaraka na kuwasahau wanyonge ambao kila mwaka huanguka mikarafuu kwa kujiatia kipato lakini pia kujenga uchumi wa nchi hii.
ReplyDeleteTuwaoneni wananchi kwa kuwajengea miundo mbinu ya kisasa kabisa ili nao wajisikie kwamba wana nchi wana viongozi wanaowajali. Wazanzibari ni watu wanyonge na maridhia sana, tusitumie mwanya huu kuwakandamiza jamaniii viongozi wetu.
Nakutakieni uongozi mwena kwa faida ya wananchi w nchi hii amiiin.
Assalaam alaykum
ReplyDeleteTunakushukuru muandishi kwa kutulea habari hii. Lakini tunakusihi heb jaribu kutumia vizuri taaluma yako ya uandishi, ingependeza kama ungetuelezea vipi hii bandari imeimarishwa. Mimi sipo Pemba kwa sasa mara ya mwisho kuitumia gati hii ilikuwa 2005/2006, lakini nikiiangalia kwenye hiypo picha sioni chochote kipya. Kimeboreshwa nini hapo tunaomba tupe maelezo.
Hivi hii ndio gati ya kujivunia kwamba tuna gati, kweli viongozi wa nchi hii wanatudhalilisha wananchi, na zaidi kwa sababu wao hasa hawatumii miundo mbinu kama hii. Kwa hiyo hata hawajali kabisa. Wanyonge wengi ndio wenye kutumia huduma kupitia miundo mbinu kama hii. Yasikitisha kweli karne ya 21, tunakuwa na mfano wa baraza ndio tunaita gati??!!. Tumuogope allah, iko siku tutarejea kwake na tutaulizwa. Viongozi wetu tumcheni allah, jamani hii ni idh-laaal kwa wananchi.
@ Anonymous 1 &2
ReplyDeleteAhsanteni kwa Machango wenu na maneno yenu mazima kabisa.... Kwanza napenda kumpa POle sana huyu Mpiga Picha wa Gazeti hili la Othmani Maulidi kwakuwajejea Wapemba kuhusu Bandari ya Wete... Hivo kweli yeye hawezi kutofautisha jinsi ya Bandari iliojengwa na isiojengwa?..
Hivo mtu anafika kupiga picha za magazeti hajui Kizuri na Kibaya?.... Au ndio Nyiye Waandishi wa Zanzinews, munaandika habari kama Makasuku tu.. Hamuna Critics wala ukweli.. Munaripoti kama vile Makasuiku...
Ninavojua waandishi wa habari na Wapiga picha wao wanatakiwa wao wawe mstari wa mbele kuandika ukweli na kuripiti mauvu na mema yanayotendeka katika visiwa vyetu..
Kufanya hivyo nikuipa Serikali motisha au viongozi wahusika waweze kutenda kazi zao kiuhakika na kwa usawa bila yakupendelea... Kwani nani asiejua kama Pemba inafanywa kama 3rd class citizen japokua wao ndio wanaotoa pato kubwa kwa uchumi wa zanzibar almost 90% ni zao la karafuu ndio linalotoka Pemba... Huo utalii Koko uliopo Unguja unasaidia 2% tu kwasababu 8% yote inachukuliwa na Viongozi pamoja na Wataliano ambao wana hisa ndani ya Utalii huo... Nyengine inakwenda kwenye Watanganyika na Wakenya ambao wana ajiriwa katika mahoteli..
Kinachonishangaza nikwamba Kisiwa cha Pemba Viongozi wa SMZ wameshindwa kukiongoza kwa usawa kama inavotakiwa. Mpaka sasa hakuna hata Univercity moja Pemba watu wakisema Wamakunduchi Wanakuja juu. Wapemba wakitaka Kisiwa chao hawapewi.... Haya yana mwisho... Mtoto unapomlea ukamkosesha haki zake mwisho atakujakukua na atakutupa weye uliekua unamlea..
@Mchangiaji wa 4
ReplyDeleteHakuna ubishi hio bandari kusema imeimarishwa huo ni utani na dhihaka kubwa. Hata hivyo, mchangiaji naona amechangia kwa jazba mpaka kuwashusha daraja wa Pemba. Kwa maoni yangu mimi wa Pemba ni watu wa daraja la juu hapa Zanzibar lakini wao hawajitambui. Wapemba ndio wanaongoza Zanzibar. Rais ni
Mchokocho na Makamo wake wa kwanza ni mpemba wa Mtambwe. Aidha, asilimia kubwa ya wasomi na matajiri wa Zanzibar ni wa Pemba. Pia nakubaliana na wewe kuwa Pemba hakuna University hata moja lakini kafanye utafiti wanaosoma katika University hizo na uje utupe majibu watumbatu, wapemba, wamakunduchi, wanzanzibara wepi ni asilimia kubwa? Kuhusiana na uchumi unaotokana na zao la karafuu naona hujatuwekea wazi nani wanafaidika nalo? Baada ya kuongezwa bei zao la karafuu kwa wakulima wa Pemba tulitegemea kuwe na mabadiliko ya maendeleo huko. Kwa sababu kutokana na utalii koko Unguja kuna significant change unayoiona huko east na north coast.
Mwisho kwa kumalizia, maendeleo ya Pemba yataletwa na wapemba wenyewe kwa kujipanga vyema na kutumia raslimali vizuri zilizoko huko kuijenga Pemba badala ya kuziekeza sehemu nyengine. Kwa kufanya hivyo Pemba itakua na university zake, beit el ajab yake, gati nzuri, forodhani na darajani yake. Chuki, ubaguzi, siasa muda wote havitasaidia Pemba na wa Pemba.
Assalaam akaykum
ReplyDeleteShukran Mchangiaji wa 6 hapo juu. Umechangia kwa weledi mkubwa na busara bila jazba kwa lengo la kuelimisha. Ila kuna points naomba niziweke sawa, kwa kipindi ambacho bei ya karafuu imeimarishwa kwa wakulimasidhani kama kweli inaweza kuleta significant changes za kimaendeleo, kweli imesaidia sana kwa wananchi individually kimaisha, lakini si kusema kwa ongezeko hilo la bei ya karafuu wananchi waweze kuboresha miundo mbinu kama hiyo ya gati, au ujenzi wa University. Mambo kama haya nafikiri bado ni wajibu wa Serikali kuwa na mikakati na dhamira ya kweli ya kuwasaidia wananchi.
Ila mimi point yangu ni kwamba kwa uwezo na usomi wa wananchi wa Pemba, bado nafikiri hatujakusudia kidhati kuisaidia Pemba kunyanyuka kiuchumi. Kuna mengi yanaweza kufanywa na wafanyabiasha/matajiri/na wasomi wa Pemba kusaidia maendeleo na ustawi wa watu kisiwa cha Pemba. Mfano kweli tunashindwa kujenga shule za Maana za sekondari na hata vyo vya elimu ya juu vyenye hadi ya kutambulikana?? Hivi kweli tunashindwa kwa kushirikiana kujengwa Hostipali za level ya wastani tu ili kusaidia waananchi wa Pemba na kuacha kusumbuka kufuatilia huduma za kiafya nje ya Pemba (nafikiri tunaweza, tukikusudia).
Na yakifanyika ha kutoka kwa wazalendo wenye ari ya nchi yao hata hii serikali itatahayari kabisa na kujirekebisha ( kama haitaweka vikwazo lakini).
Nawaomba wazalendo kutoka Pemba na Zanzibar kwa ujumla tushirikiane kuleta maendeleo yetu wenyewe kwani serikali kwa mwenendo tuonaouona itachukua muda mrefu sana kufanikisha malengo na ndoto zetu za maisha bora.