Habari za Punde

Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Ubungo Modern ya Dar es salaam walipotembelea maeneo ya Kihistoria Zenj

 
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kutoka Makao Makuu Dar es Salaam Stella Vuzo akitoa ujumbe wa siku ya Kimataifa ya kumbukumbu ya wahanga wa Utumwa na Biashara ya Utumwa ngambo ya Bahari ya Atlantiki kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Ubungo Modern (hawapo pichani) walipotembelea maeneo yaliyokuwa yakiendesha Biashara ya Utumwa Zanzibar.
 Mtembezaji wageni Peter Mashauri wa Kanisa la Mkunazini akiwapa maelezo wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Ubungo Modern ya Dar es salaam walipotembelea maeneo ya Kihistoria yaliyokuwa yakiendesha Biashara ya Utumwa Zanzibar katika siku ya Kimatafa ya kumbukumbu hiyo inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi, 25 .

 Wanafunzi wa Sekondari ya Ubungo wakimsikiliza mtembezaji wageni (hayupo pichani) wakiwa katika chumba kidogo kilichokuwa kikihifadhiwa watumwa waliokuwa wakisubiri kusafirishwa kwa ajili ya kupigwa mnada katika Kanisa Kuu la Mkunazini.


Wanafunzi wa Ubungo Modern wakiangalia vitabu vya Historia ya Zanzibar walipotembelea Kasri ya  Wananchi  Forodhani Mjini Zanzibar


 Wanafunzi wa Ubungu wakipata maelezo kutoka kwa mtembezaji wageni Peter Mashauri wa Kanisa la Mkunazini walipotembelea magofu ya kuhifadhia watumwa yaliopo Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Wanafunzi wa Ubungo wakiangalia sehemu waliyokuwa wakihifadhiwa watumwa katika maeneo ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Wanafunzi wakiangalia Bandari ndogo iliyokuwa ikitumika kupokelea na  kusafirisha watumwa katika maeneo ya  Mangapwani Mkoa Kaskazini Unguja.

(PICHA NA MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR.)


3 comments:

  1. hizi historia za uongo mtaziacha lini? watumwa walipitia zanzibar kutokea bara kuelekea majuu nchi za karibeani na amerika huko ndiko walikuwa wakipelekwa kwenda kufanya kazi katika mashamba ya wakoloni wa ulaya , hakuna mwananchi hata mmoja mzanzibari alipelekwa utumwani. Hao watu wa makanisa ndio waliotuletea huu utumwa walikuja mwanzo wakijidai ni wamishenari kumbe wapelelezi wa kutafuta maeneo ya rasilimali , na kuwatayarisha watu wetu kiroho kukubali kutawaliwa. Utumwa haukupigwa vita na makanisa yoyote yale msitudanganye , biashara ilikufa yenyewe kwa ajili ya ukuaji wa machine na viwanda ambavyo havihitaji watu ( industrial revolution ) .Waarabu walikuwa ni watu wa kati middleman katika hio biashara wakiwatumikia wakoloni kuwapelekea watumwa ambao wengi walikuwa ni wafungwa wa kivita katika vita vya machifu vinapotokea katika vijiji na walikuwa wakiuzwa na machifu wenyewe. Waarabu walitumiwa kwa kuwa walikuwa wameshaingiliana na wananchi wa afrika na kuchanganyikana nao , pia wakijua njia za kupita wakati ule hakukuwa na barabara . Kwa kifupi biashara ya utumwa ilianzishwa na wakoloni na ilikufa kutokana wakoloni waliendelea kiufundi kwa hio hawakuhitaji waafrika tena kuwafanyia kazi. Ushahidi mkubwa ni umati wa watu wenye asili ya kiafrika katika nchi za karibean na amerika , walifikaje kule? Waarabu hawakupeleka watumwa arabuni , wakitoka zanzibar walikuwa katika bahari hubadilishwa chombo walichopanda na kupakiwa vvyombo vya wakoloni kuwapeleka maeneo niliyotaja hapo juu.

    ReplyDelete
  2. Historia ya Zanzibar inatolewa na mtu wa Tanganyika! si angalitafutwa mtu wa visiwa hivi au ndio ukoloni mambo leo

    ReplyDelete
  3. @ Anonymous 1
    Ahsante ...lakini Usishangae na hizo Historia za Uongo.. Umesikia Mtembezaji anaitwa Peter Mashauri utategemea nini???

    Mimi nashangaa Kanisa la Mkunazini limetekwa Nyara na Wakurya , na hao ndio wanaotia Propagander za Uislamu na Ukristo... Mimi nina rafiki yangu alikuja Unguja kutembea na habari alizozipokea aliambiwa kwamba Waarabu na Uislamu ndio Walioleta Watumwa...

    Sasa huko Vijijini Kwao Unyikani ni Nani aliweza kuwakamata? Sio wao wenyewe kwa Wenyewe akina Marchifu Mkwawa sijui Madenge...n.k

    Masuala ya Historia za Miji na makanisa ya Mji Mkongwe yanatakiwa waachiwe Municipal ya Zanzibar hizo ndizo kazi zao... Lakini Ndio hivo tena Wasomi wamefukuzwa manispaa na Wamewekwa hata watanganyika.. Mbona Municipaa zao kule Bara hawaweki Wazanzibari?..

    Sasa hilo kanisa linaingiza Hela ya kigeni na hao Mapadiri au Paparazi ( Akina Peter ) Hawawezi kulitengeneza.. Hivo pesa wanazifanya nini... Hao ndio watakao kua Maraisi wetu 2020... Mapadiri na watembezaji wa Kitanganyika... hivo ghakuna Wazanzibari wanaojua historia ya Mji mkongwe mpaka wachuliwe watwana....?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.