Habari za Punde

Bonaza la Ziro 3 Kupambana na Maambukizi ya Ukimwi Zanzibar Viwanja vya Amani.

Mwenyekiti wa Baraza la Maichezo Zanzibar BMZ Bi Sherry Khamis, akizindua Bonaza la Ziro Tatu kwa Vijana Kupiga Vita Maambukizo ya Ukimwi Zanzibar,akirusha mpira kulizindua kwa mpira wa peti, Bonaza hilo limeandaliwa na Jumuiya ya ZAYADESA, katika viwanja vya amani nje.
Mratibu wa miradi wa ZAYEDESA nDG. Mgoli Lucian akielezea madhumuni ya Bonaza hilo la Ziro Tatu , na kutoa maana ya ZIRO TATU, ziro ya kwanza ni Kuondoa Unyanyapaa, Ziro ya Pili Kupunguza Vifo kwa Maambukizo ya Ukimwi na Ziro ya Tatu kupunguza na kuondoa Maambukizo kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto Zanzibar. Bonaza hilo limefanyika viwanja vya nje uwanja wa Amani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi. Sherry Khamis, akitowa nasaha zake kwa Vijana wanamichezo walioshirika Bonaza hilo, na kushirikisha michezombalimbali ya Vijana kuhamasisha kuondoa maanbukizo ya Ukimwi kwa Vijana wa Zanzibar. 
Katibu wa Jumuiya ya ZAYEDESA Bi. Lucis Majaliwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bonaza hilo lililozinduliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar, katika viwanja vya nje Amani Zanzibar, jumla ya Vijana 400, wameshiriki katika Bonaza hilo. 
Washiriki wa Bonaza hilo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar akitowa nasaha zake.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi. Shery Khamis akiwasalimia baadhi ya Wanamichezi walioshiriki Bonaza hilo baada ya kulizinduwa katika viwanja vya Amani Zanzibar.
Mratibu wa Miradi wa ZAYEDESA Ndg. Mgoli Lucian, akiongozana Wafanyakazi wa ZAYEDESA, kuwasalimia wanamichezo walioshiriki Bonaza hilo la Ziro Tatu.katika viwanja vya Amani. 
Washiriki wa Bonaza la Ziro Tatu, wakishiriki mchezo wa netiboli kati ya timu ya Amani na Mpendae, Mchezaji wa timu ya Mpendae akiwa na mpira huku mchezaji wa timu ya Amani, timu Mpendae imeshinda 15--9 


Mchezaji wa timu  ya Netiboli ya Mpendae akiwa na mpira akijianda kutowa pasi kwa mwezake,katika mchezo wa Bonaza la ZAYEDESA Z iri Tatu lililofanyika viwanja wa Amani Nje.timu ya Mpendae imeshinda 15-9 


Wasanii wa kikundi cha Magogoni Zanzibar wakionesha mchezo jinsi ya kujingia na kupambana na Maambukizo ya Ukimwi, onesho hilo limefanyika katika michezo ya Bonaza la Ziro Tatu  
Vijana wakifuatilia michezo ya Bonaza la Ziro Tatu kuhamasisha kupiga Vita maambukizo ya Ukimwi kwa Vijana, jumla ya Vijana 400 wameshiriki Bonaza hilo kwa michezo mbalimbali Mpira wa Miguu, Netibo, Basketi Ball, Kuvuta Kamba, Wasanii wa Zenj Flava, Michezo ya Maigizo na Sanaa mbalimbali. 
Wasanii wa michezo yav Kuigiza kutoka Magogoni wakionesha michezo ya kuepeka na Maambukizo wa Ukimwi kwa Vijana.
Wasaii wa Kizazi Kipya Boys Six,wakionesha umahiri wao wa kudensi muziki wa Zenj Flava wakitowa burudani katika Bonaza hilo lililofanyika viwanja vya Amani nje Zanzibar. 















No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.