Na
Kadama Malunde, Shinyanga
ASILIMIA
kubwa ya watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino), wanaolelewa katika kituo cha
Buhanghija kilichopo mjini Shinyanga, wametelekezwa na wazazi wao kiasi cha
kufikia hatua ya watoto hao kutosherehekea sikukuu ya pasaka.
Hayo
yameelezwa na mwalimu mlezi wa kituo hicho, Maisala Adinani, wakati familia ya
Anna Mwalongo ya mjini Shinyanga, ilipotoa msaada wa chakula kwa watoto hao kwa
ajili ya kusherehekea sikukuu ya pasaka.
Alisema baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo
hicho wakiwemo wasiosikia na wasioona, tayari wamechukuliwa na wazazi na walezi
wao kwenda kusherehekea sikukuu ya pasaka lakini kwa upande wa watoto wenye
ulemavu wa ngozi, hakuna mzazi wala mlezi
yeyote aliekwenda kuwatembelea
wala kuwachukua watoto hao.
Alisema
wakati wa sikukuu baadhi ya watoto wenye ulemavu huchukuliwa na wazazi wao,kama walivyofanya kipindi hiki lakini watoto wenye
ulemavu wa ngozi hubaki katika kituo hicho siku zote.
Nayo
familia ya Mwalongo iliyotoa msaada wa chakula kwa watoto hao, imeelezea
kuguswa na watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu na kuongeza kuwa iliona
si vyema kusherehekea sikukuu ya pasaka peke yao na kuamua kuwatembela watoto hao.
Anna
Mwalongo na Josephat Mwalongo ambao ni wanafamilia, walisema jamii inapaswa
kutambua kuwa watoto hao ni wa wote na sio kukiachia kituo hicho kila kitu.
“Tumeona
ni vyema kuwatembelea na kuwasaidia chakula watoto hawa pamoja na kambi ya
kulelea wazee wasiojiweza ya Kolandoto iliyopo mjini Shinyanga, ili wasione
kuwa jamii imewatenga kama walivyoachwa na wazazi wao,” walisema.
Familia
hiyo haikuishia kutoa msaada katika kituo hicho tu, pia ilitoa msaada katika
kambi ya wazee ya Kolandoto.
No comments:
Post a Comment