Na
Mwandishi wetu
RAIS
Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya mazungumzo
na majadiliano ya kina na viongozi wa vyama vyote vya wafanyakazi nchini yenye
nia ya kutafuta njia za kuboresha maslahi na ustawi wa wafanyakazi.
Mazungumzo
hayo ya muda mrefu yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam yalihudhuriwa pia na
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
(Utumishi), Celina Kombani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa
Ghasia, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni
Sefue.
Aidha,
mazungumzo hayo yalihudhuriwa na maofisa waandamizi wa serikali wakiwemo
Makatibu wakuu wa wizara ambazo zinahusika moja kwa moja na maslahi na ustawi
wa wafanyakazi na uongozi wa vyama vya wafanyakazi uliongozwa na uongozi wa juu
wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA).
Rais
Kikwete na viongozi hao kwa zaidi ya saa 10 walijadili hali ya utekelezaji wa
masuala na mambo yaliyokubaliwa katika kikao chao cha namna hiyo kilichofanyika
Februari 27, 2013.
Iidha
Rais Kikwete na viongozi hao wakiwemo wale wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)
walichambua kwa kina hoja za wafanyakazi zilizowasilishwa kwa Ikulu na vyama
hivyo.
Miongoni
mwa hoja hizo ni ajira kwa wageni na athari zake kwa ajira ya Watanzania,
athari za kuzuka kwa mawakala wa ajira, watumishi waandamizi wa serikali
kushikilia nafasi za uongozi katika vyama vya wafanyakazi na athari zake,
ushirikishwaji wa wafanyakazi katika
bodi za taasisi za umma na serikali na uhamisho wa maofisa kazi ambao Rais
Kikwete aliuagiza miaka mitatu iliyopita.
Hoja
nyingine zilizojadiliwa ni hali ya afya ya wafanyakazi katika migodi nchini,
bei ya umeme majumbani na athari yake kwa wafanyakazi, uwezekano wa kupunguza
tena kodi kwenye mishahara ya wafanyakazi jambo ambalo serikali ililifanya mwaka
2013, madai ya malimbikizo ya mapato ya wafanyakazi, madeni ya walimu na uwezekano
wa nyongeza ya mishahara kwa walimu.
Katika
kikao hicho, Rais Kikwete aliagiza wizara, idara na taasisi zote za serikali na
umma ambazo hazijatekeleza mahitaji ya kisheria ya kuundwa kwa mabaraza ya
wafanyakazi katika utumishi wa umma kufanya hivyo mara moja bila kuchelewa.
Alitoa
muda hadi Mei mosi mwaka huu kwa wizara, idara na taasisi hizo kuwa tayari
zimeunda mabaraza hayo na alimwagiza Balozi Sefue kutuma barua za maagizo ya
Rais kwa wizara, idara na taasisi inayohusika.
Aidha
alisema mwishoni mwa mwaka huu, atapenda kupata taarifa kuhusu hali ya
uanzishwaji na utendaji wa mabaraza hayo ambayo ni muhimu kwa uwakilishi wa
wafanyakazi katika uendeshaji wa taasisi za umma ambazo wanazifanyia kazi.
mambo ya katiba yamemchachia JK alitaka kutumeza zanzibar , sasa anatafuta ushirikiano kwa wafanyakazi kwa kuwaahidi kuongeza mishahara nk hii kama sio rushwa ni nini Ndugu Rais? harakati zako zote zitaishia bandarini darisalama bwana mkubwa , huku visiwani mmetushika mkono , ukila na kipofu usimshike mkono , mshafanya hilo kosa haturudi nyuma mpaka tupate uhuru kamili wa visiwa hivi , ikiwa sheni na timu yake haikubaliani na sisi wananchi tunawaomba wahamie tanganyika ,
ReplyDelete