Na
Masanja Mabula, PEMBA
KIKOSI
maalumu cha kuzuia magendo (KMKM) kisiwani Pemba ,
kimekamata magunia 34 ya karafuu kavu ambazo zilikuwa katika harakati ya
kusafirishwa kwenda nje ya nchi kwa njia ya magendo.
Kamanda
wa KKMK kamandi ya Pemba, Silima Haji Haji, alisema karafuu hizo zimekamatwa
katika bandari bubu ya Gome iliyoko Kinowe Micheweni usiku wa kuamkia Jumapili
majira ya saa nane usiku.
Alisema
karafuu hizo zimekamatwa na askari wa kikosi
hicho kambi ya Msuka kwa kushirikiana na wale wa makao makuu ambao walikuwa
katika doria zao za kawaida.
Alisisitiza
haja kwa wananchi kuendelea kuuza karafuu zao katika vituo vya Shirika la Taifa
la Biashara (ZSTC) ambalo limepewa jukumu na serikali la kununua karafuu na
kujiepusha na biashara ya magendo.
Alisema
wafanyabiashara wa magendo ya karafuu hawana nia njema na uchumi wa nchi kwani
wanachojali ni maslahi yao
binafsi na kuwataka wananchi kuepukana nao kwani wanaikosesha mapato serikali.
Hii
ni mara ya tatu kwa kikosi hicho kisiwani hapa kuzima majaribio ya utoroshwaji
wa karafuu kavu kwenda nje ya nchi kwa njia ya magendo ambapo kwa kipindi cha
mwaka huu magunia 118 yamekamatwa.
ikiwa bei mnayotoa ni ndogo mnataka wakulima wakuuzieni kwa bei ya kutupa , wala hawafanyi magendo yoyote wanajaribu kupelea bidhaa zao sehemu ambako watapata thamani kamili ya nguvu zao , mnawadhulumu tu , serikali ilichitakiwa ni kuweka bei inayofanana na hio ya masoko ya nje ili wakulima wavutiwe kuuza hapa hapa nchini , na tunaweza hata KMKM tukaifungilia mbali wala haina haja ikiwa tunatumia mamilioni kuwaajiri hawa KMKM , kwa nini tusiondoe KMKM halafu fedha zikaelekezwa kuongeza bei kwa wakulima?
ReplyDelete