Habari za Punde

Mufti Mkuu Z’bar asikitishwa na matusi bunge la katiba

Na Mwandishi wetu
WAJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba, wametakiwa kuzingatia kile kilichowapeleka Dodoma badala ya kuendeleza lugha za kejeli na matusi.

Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi, alielezea wasiwasi wake juu ya lugha za matusi zinazotumika katika mjadala huo ambao kwa kiasi kikubwa ni kinyume cha maadili ya dini zote ambazo zinahimiza kuheshimiana na kutodharauliana.

Mufti Kaabi alikemea tabia iliyojitokeza katika bunge hilo ambapo wabunge wamekuwa wakitukanana matusi ya nguoni na kusahau kwamba Watanzania wanachotegemea kutoka kwao ni michango ambayo itaboresha rasimu hiyo ya katiba iliyo mbele yao.

Alisema kwamba Watanzania wanachotegemea kutoka kwa wajumbe hao ni hoja za msingi katika kutetea misimamo yao na sio kutukanana na kukejeliana.

Aliwataka wajumbe hao wavumiliane pale ambapo mjumbe atasikia hoja ambazo hazitamridhisha na ajiandae kujibu hoja hizo kwa dalili zenye mishiko.


Mufti Kaabi alikitakia kheri kikao hicho ili kifikie makubaliano juu ya katiba muwafaka inayotarajiwa na Watanzania wote.

6 comments:

  1. tatizo nnaloliona kwa huku kwetu znz mipasho ndio siasa yetu na kuwabadilisha wanasiasa ni kazi ngumu maana wanasiasa wanaangalia maslahi yao na wajipendekeza kwa wale wanaowapa vyeo

    ReplyDelete
  2. Wahenga walisema mzoweya punda hapandi farasi na mh. Tundu lissu nae akasema mzoweya vya haramu vya halali haviwezi, hawa ndio ndugu zetu wa CCM Zanzibar wameshazoweya siasa za matusi,ubaguzi,kejeli unafkiria wataweza kujenga hoja kweli na wao hawajawahi maisha mwao kuongelea hoja za msingi zenye mustakabi mzuri kwa nchi yetu. Kwahio mimi sishangai sana maana mzoweya punda hapandi farasi.

    ReplyDelete
  3. Wahenga walisema mzoweya punda hapandi farasi na mh. Tundu lissu nae akasema mzoweya vya haramu vya halali haviwezi, hawa ndio ndugu zetu wa CCM Zanzibar wameshazoweya siasa za matusi,ubaguzi,kejeli unafkiria wataweza kujenga hoja kweli na wao hawajawahi maisha mwao kuongelea hoja za msingi zenye mustakabi mzuri kwa nchi yetu. Kwahio mimi sishangai sana maana mzoweya punda hapandi farasi.

    ReplyDelete
  4. Wahenga walisema mzoweya punda hapandi farasi na mh. Tundu lissu nae akasema mzoweya vya haramu vya halali haviwezi, hawa ndio ndugu zetu wa CCM Zanzibar wameshazoweya siasa za matusi,ubaguzi,kejeli unafkiria wataweza kujenga hoja kweli na wao hawajawahi maisha mwao kuongelea hoja za msingi zenye mustakabi mzuri kwa nchi yetu. Kwahio mimi sishangai sana maana mzoweya punda hapandi farasi.

    ReplyDelete
  5. Mimi kilichonisikitisha zaidi Nikuona Jinsi gani CCM Tanagnyika wanavofurahia wazanzibari wakitukanana.. kama alivosema Muheshimiwa sanya. kwamba Dodoma Inawagombanisha wazanzibari.. Hii Nikweli halafu wako wale CCM-Tanganyika wanaokua wanazomea na sauti zao unazisikia..

    Hivo Mtu atawashaje spika yake wakati hajaruhusiwa kusema na mwenyekiti?..Halafu huyo Samuel Sitta mwenyewe, pinda, Seifu Ali iddi na viongozi wengi kama anna makinda wanachekelea matusi hayo..

    hii inanihuzunisha zaidi.. sisi tulipokoma ni wamoja tuna udugu wa damu kwanini tgombanishwe?...ikiwa Muheshimiwa jussa kakosea kusema Kwamba Wazanzibari "wameufyata" wangesikiliza tu halafu wakamueleza kule Nje.. sio kutukanana nakumwambia kwamba hajaoa wala hana mtoto.. kwani kila anae owa na kuolewa hupata mtoto?..Mbona mimi nimeolewa miaka na kaka lakini sijatunga hata mimba yakuharibu..

    Wanaoizamisha Zanzibar ni wazanzibari na sasa wako wengi kweli ambao hatukuwatarajia.. haya basi na lizame watakao pata shida sio wapemba wala wahindi.. ila shida ikiikumba Zanzibar itatupata sote.. Na hasa hao wanaojiita Wahadimu ndio watakao kula dhiki pindipo zanzibar ikiwa Kikata cha Mkoa wa pwani.. hivo tuko Nchi na rtunapewa 4.5% ya share zote za muungano.. jee tikiwa KATA ya Mkoa wa pwani tutapewa ngapi?

    ReplyDelete
  6. "Hasa hao WAHADIMU"- wahadimu wadabakia ni wahadimu na watoto wa nyoka watabakia ni nyoka tuuna watoto wa nge watabakia nge tuu ndumila kuwili,kutafuna huku na huku.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.