Habari za Punde

PBZ Yasaidia Kituo cha Redio cha Al Noor kilichounguwa Moto wiki zilizopita Mtoni Daraja bovu.

Meneja Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd, Ndg. Seif Suleiman, kushoto akimkabidhi Cheki Mkurugenzi Mtendaji wa Al Noor Charitable Agency Ndg Nadir Mohammed Mahfoudh, katikati kwa ajili ya kuchangia  ujenzi wa Kituo cha RedioAl Noor kilichoungua moto wiki zilizopita na kuharibika kwa Studio hiyo kuteketea kwa moto. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Redio hiyo Masjid  Noor, Mtoni darajabovu.
Mkurugenzi  Masoko wa PBZ Ltd, Ndg. Seif Suleiman, akizungumza katika hafla hiyo ya kukubidhi Cheti kwa ajili ya kuchangia Redio hiyo iliopata ajali ya Moto wiki zilizopita na kuleta madhara ya kituo hicho na kuungua kwa Studio zake, kutokana na moto huo.Na kuzitaka taasisi nyengine kuchangia Redio hiyo ili kuweza kurudisha huduma zake za matangazo kwa Jamii. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Al Noor Charitable Agency Ndg Nadir Mohammed Mahfoudh, akitowa shukrani kwa Uongozi wa PBZ kwa msaada wao kuweza kufanikisha kuchangia Kituo hicho kuweza kurudisha huduma za matangazo ya redio yao iliopata majanga ya moto. 
Na kusema kituo cha kinahitaji shilingi milioni thamani ili kuweza kurudi hiwani kwa kupata vifaa vilivyoharibiwa na moto huo. Amesema wako katika jitihada za kutafuta fedha hizo kuweza kurudisha huduma hiyo kwa Wananchi wa Zanzibar na vitongoji vyake.
Kwa sasa wanatumia kituochao cha kurushia matangazo cha masingini kuweza kurusha matangazo. Na kuwataja Waumini wa Kiislam na Wananchi kwa kutowa michango yao kuweza kufanikisha kukamilisha fedha hizo kununua vifaa vilivyoharibika na moto huo.


Mkurugenzi wa RedioAl Noor, Shekh. Mohammed Suleiman Tall, akizungumza katika hafla hiyo na kutowa maelezo ya tukio hilo na jinsi mmoja wa Mfanyakazi wa kituo hicho aliekuwa zamu wakati wa jali hiyo kuumia na sasa yuko katika hali ya hujambo na naendelea na matibabu katika hospital kuu ya mnazi mmoja.


Meneja Masoko wa PBZ Ndg. Seif Suleiman akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Redio Al Noor Mohammed Suleiman Tall, alipotembelea redio hio kukabidhi msaadawao.












No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.