Habari za Punde

Wenyeviti wa UKAWA Wazungumza na Waandishi wa Habari Zenj.

Viongozi wa UKAWA wakiwa katika mkutano na Waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Mzsons Shangani Zanzibar baada ya mkutano wao kuahirishwa na jeshi la Polisi Zanzibar kwa sababu za kiusalama .
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwa katika ukumbi wa mkutano na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimnali viliko Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Chama cha CUF Mhe. Profesa Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kutoka kwa Wajumbe wa UKAWA kutoka Vyama vya Upinzani Wanaohudhuria Bunge Maalum la Katiba 
Mwenyekiti wa  CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe, akizungumza na waandishi wa habari sababu za kutoka katika bunge maalum la katiba Tanzania.akisisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa hoteli ya Mazsons shangani Zanzibar.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe. James Mbatia akizungumza na waandishi katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Zanzibar.





  Baadhi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba wakimsikiliza Kiongozi wa UKAWA Mhe. Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteliya Mazsons ukumbi wa mlingoti.
Baadhi wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa UKAWA waliotoka katika Kikao cha Bunge hilo wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Shangani Zanzibar wakizungumza na waandishi wa habari.

7 comments:

  1. Bungeni ni pahala pakujenga hoja sio nje ya bunge. Ujinga wa mtu kukosa akili.

    ReplyDelete
  2. Bunge gani lisokuwa na heshima wanakaa wakibagua muarabu atarudi wanajua warabu wanaishi vipi huku mimi nina watoto nikiwambia tukatembea tanzania anakujibu baba kunanuka

    ReplyDelete
  3. Hao wanaojiita ukawa nahisi hawajui kilichowapeleka bungeni km wangejua kilichowapeleka huko wasingegoma. Utamu wa ngoma uingie ucheze. Hicho wanachotaka kitufikie wananchi wangekisema wakiwa ndani ya bunge km kweli wao wanauchungu na nchi. Wasitufanye viini macho . Utatuzi wa tatizo haupatikani kwa kugonma . Bora warudi bungeni ndio tutawaelewa. Kwa sasa hatuwaelewi maana sucho wananchi tuluchowatuma.

    ReplyDelete
  4. wametoka tuko pamoja sasa pale wanajadili nn zaidi ya matusi bunge huyu muhindi mpemba kaoa hajaolewa ndio bunge hilo

    ReplyDelete
  5. kama kweli wana uchungu na wananchi wangebaki bungeni na kutetea maslai ya wananchi. kama in matusi mbona hata wao walikuwa wanatoa matusi. Sielewi ni mantiki gani Wametoka bungeni Labda wana agenda yao.

    ReplyDelete
  6. wanataka kutunga katiba ya ccm sio ya wananchi ndo tatizo chama cha kifsadi ccm

    ReplyDelete
  7. ikiwa nyinyi wazanzibari hamjaona kutukanwa na lukuvi basi vipofu kweli kweli wala mungu asikujaalieni kuona ukweli akuacheni na upotofu wenu mmbakie tukutawaleni

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.