Habari za Punde

Harakati Marikiti ya Mkokotoni Unguja

Wananchi wakiwa katika harakati za hapa na pale katika marikiti kuu ya Mkokotoni Unguja Wiala ya Kaskazini A, Marikiti hii hutowa huduma kwa wananchi wa Kijiji hicho na kisiwa cha Tumbatu. kupata mahitaji yao.    

4 comments:

 1. Huyo Mbunge na Mkuu wa Mkoa wa Huko Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A.. Kwanini Wasiwajengee Wananchi Marikiti ya Kisasa kama vile Bazar au Shoping Moure??? Mapesa wanayapata mengi na wanapita wakiwadsanganya watu kila baada ya miaka 5 kwamba watawaletea Maendeleo.. Marikiti hiyo Ilio Oza kama ile ya Darajani inaweza kubadilishwa kama Viongozi na Wananchi wao wana Vission ..

  ReplyDelete
  Replies
  1. Viongozi wameoza na wamewaozesha na wananchi wao, hata tukijengewa soko jipya la kisasa kabisa, bado nakwambia tutauza bidhaa chini au nje ya soko. Hawa wakubwa wetu hawa vision yoyote, kutwa wako nje ya nchi lakini sijui ndio hawayaoni maendeleo ya watu katika nyanja kama hizi za kibiashara, kwa wenzetu ukienda katika maeneo ya biashara utapenda hasa, kila kitu kiko kwa mipangilio mizuri kabisa. Maduka yamepangwa vilivyo, bidhaa safi na ziko kwa mpango maalum. Hapa kwetu, unaweza kuona soko la samaki na hapo hapo kuna jaa, kuna garage, kuna skuli mambo tirigivyogo tuuu.

   Delete
 2. Hawa ndio tushawazoea lkn mm nashangaa zaidi nikiwaona hawa ninaowatarajia kuwa ni watetezi wetu na ndio viongozi mbadala. Pemba yote inaongozwa na wabunge na wawakilishi pamoja na madiwani kutoka CUF kwa takribani miaka 20 sasa.Lkn hiyo hali unayoiona Mkokotoni haina tofauti na ya majimbo hayo ya Pemba.

  ReplyDelete
 3. Kwani Zanzibar kuna Marikiti au masoko?? Mimi naona ni vipenu tu, watu huanza kutarazzak kwa kuuza matunda n.k pembeni kabisa mwa barabara, baada ya muda biashara hukua na hatimae kuzoeleka eti ni Soko au Marikiti. Kweli kazi tunayo. Hivi pale Mkokotoni na kwengineko Zanzibar zile ndio marikiti. Hata ile ya Darajani ni aibu tupu wallah, ukija na mgeni wako Zanzibar, nakwambia ni aibu kabisa, hujua soko ndio ipi, mambo ovyo ovyo tuu. Pita sasa hivi Darajani, uone watu wanauza bidhaa chini kabisa, wengine juu ya mifuniko ya makaro ya mji mkongwe!! Tuna tatizo kwa kweli, suala la biashara Zanzibar, inashangaza sana kwamba bado tuko nyuma katika kila aspect, ukianzia usafi wa mazingira ya biashara, mipangilio mibovu ya sehemu za kufanyia biashara. Nenda Malindi soko la samaki, nenda Nungwi soko la samaki, watu wameacha kuuza bidhaa (samaki) ndani ya masoko na badala yake wanauza chini kabisa (Chini ya Mkungu pale Nungwi), Malindi wanauza nje ya soko chini kabisa na kila mmoja wetu anaona. Sijui tuna maradhi gani?
  Sijui ndio mapuuza au tumechoka na maisha... Allahu a'allam

  ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.