Habari za Punde

Tindwa asifu utekelezaji awamu ya pili ya TASAF Pemba

Na Abdi Suleiman, Pemba
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Juma Kassim Tindwa, amesema mikoa ya Pemba ni sehemu ya mikoa ya  Tanzania, iliyofanya vizuri katika mradi wa TASAF awamu ya pili na kubahatiaka kuendelea na miradi mengine inayofadhiliwa na TASAF.

Aliyaeleza hayo wakati akifungua mafunzo ya siku 10  kwa wawezeshaji kuhusiana na kaya masikini kisiwani Pemba  katika ukumbi wa Tassaf Chake Chake.

Aliwataka wawezeshaji hao kuendelea kuipatia sifa kubwa Pemba katika kutoa kwao taaluma na kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo.

Alisema  wananchi wana matumaini kwamba TASAF awamu ya tatu itatoa matunda bora zaidi yatakayosaidia kupunguza kasi ya umaskini.

Alisema mpango huo wa kunusuru kaya masikini zipatazo milioni 1.2 zilizo katika mazingira magumu na hatarishi kwenye vijiji, shehia na mitaa, unalenga kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira mazuri.


Kwa upande wake, Meneja Msajili ya Walengwa, Phillipien Mmari, alisema awamu ya tatu ya amradi huo utakamilika mwaka 2012.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.