UKOSEFU wa huduma ya umeme kwa
baadhi ya maeneo wilaya ya Buliisa nchini Uganda, kumesababisha wenye biashara
kama vile wauza mafuta sheli, kutumia mkonge wa kuzungusha kwa mkono, kama muuza
mafuta ambae hakupatikana jina lake, alivyokutwa na mpigapicha wetu (picha na Haji Nassor, Kampala)
MIONGONI mwa fursa za kimaendeleo ambazo wananchi wa wilaya za Hoima na Buliisa Magharibi mwa Uganda wameanza kuzipata, hata kabla ya uchimbaji wa mafuta kuanza rasmi, ni kuanza kujengewa barabara inayokwenda moja kwa moja kwenye eneo linalotayarishwa kwa ajili ya kumwagia taka taka za mafuta machafu machafu pamoja na maeneo y vijiji vya Ngege, Kasemene na Masindi kwenye visima vya mafuta (picha na Haji Nassor, Kampala)
MTAALAMU wa kimataifa kutoka kampuni ya ‘ENVIRO
SERV’ ya Afrika ya kusini Grant Coroine, ambayo kampuni hiyo imeanza harakati
za awali, za kujenga madampo maalumu ya kuhifadhia taka taka za mafuta machafu
nchini Uganda, akizungumza na waandishi wa habari wa Tanzania, Ghana na Uganda,
wakati walipofika hapo kuona hali ya ujenzi inavyokwenda, ambapo nchi ya
Uganda, ikitarajia kuanza rasmi kazi hiyo wakati wowote (picha na Haji Nassor, Kampala)
GREDA linalomilikiwa na kampuni ya ‘ENVIRO
SERV’ ya Afrika kusini, likiwa katika harakati za kichimba eneo ambalo
linatarajiwa kujengwa madampo (mabwa) ya kutunzia takataka za mafuta, wakati
nchi ya Uganda ikiwa imegundua mafuta magharibi mwa nchi hiyo, na wakitarajia
kuanza kuchimbwa wakati wowote na kampuni Tullow ya UK (picha na Haji Nassor, Kampala)
MKONGA mrefu ambao ndio mashine maalumu ya
kampuni ya Tullow ya UK, inayojaribu kuchimba mafuta kwa hatua za awali (oil
testing drilling) wilaya ya Buliisa nchini Uganda, jirani na ziwa Albertan
kuelekea nchi ya Jamhuri ya kidemokaria ya Kongo (picha na Haji Nassor, Kampala)
No comments:
Post a Comment