MCHAMBUZI wa sera na uongozi kutoka taasisi ya
‘Revenue watch Institute ‘RWI’ ya Marekani Marie Lintzer akiwasilisha mada juu
usisitizaji wa uwazi kwa makampuni ya uchimbaji mafuta, gesi na madini ‘EITI’
kwa waandishi wa habari 29 wa nchi za
Uganda, Ghana na Tanzania (Zanzibar) kwenye mafunzo ya kuandika habari za gesi,
mafuta na madini yanayoendelea nchini Uganda, (picha na Haji Nassor, Uganda)
MTAALAMU wa miamba na mafuta wa Idara ya
uzalishaji petroli nchini Uganda, Dozith Abeinomugisha, akijibu masuali ya
waandishi wa habari wa nchi za Ghana, Uganda na Tanzania (Zanzibar), akielezea
mikakati ya uchimbaji wa mafuta na uhifadhi wa mazingira, kwenye mafunzo
yanayoendelea ya kuandika habari za mafuta, gesi na madini nchini humo (picha na Haji Nassor, Uganda)
JIJI la Kampala nchini Uganda, limekuwa
likiwavutia wageni waliowengi, kutokana na baraza la mji huo, kujipanga vyema
kufanya usafi, kama mfanyakazi wa Baraza la Mji wa Uganda, ‘BMU’ akifanya usafi
kwenye barabra ya kuelekea Chuo kikuu cha Makerere, ambapo kwa siku barabara
hizo husafishwa mara mbili (picha na
Haji Nassor, Uganda)
WAKATI jiji la Dar-es Salaam nchini
Tanzania likipiga marufuku matumizi ya pikipiki za biashara ‘boda boda’ katikati
ya mji, jiji la Kampala nchini Uganda, ambako ndiko biashara hiyo inaelezwa
ilianzia, inaendelea kwa kasi na kuwepo kwa boda boda zaidi ya 100,000 (laki
moja) hadi sasa na kusababisha usumbufu mkubwa katikakati ya jijini hilo (picha na Haji Nassor, Uganda)
WAANDISHI
wa habari kutoka Tanzania wakiwa wameshikilia mishikaki maalumu ya mbuzi,
katika wilaya ya Hoima nchini Uganda, wakati wakipunzika eneo hilo kuelekea yanayotarajiwa
kuanza rasmi uchimbaji wa mafuta, waandishi hao pamoja na wenzao wa Uganda na
Ghana wanaendelea na mafunzo ya siku kumi nchini humo ya kuandika habari za
gesi, mafuta na madini (picha na Haji
Nassor, Uganda)
No comments:
Post a Comment