Afisa Mawasiliano na Ruzuku Binafsi Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania Ndg. Japhet Sanga, akizungumza na Waandishi wa habari wa Zanzibar kuhusiana na kufaidika na Mfuko huo kujitokeza kuomba Ruzuku katika kutafuta habari za uchunguzi, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Shangani Zanzibar.
Ndg Sanga aisisitiza jambo na kuwahasisha waandishi kutumia fursa hiyo ili kufaidika na Mfuko huo katika majukumu yao ya kutafuta habari sehemu mbalimbali za Zanzibar na Vijiji kuibua habari za uchunguzi .
Waandhishi wa habari wakifuatilia mafunzo hayo ya kuibua habari za uchunguzi wakimsikiliza Muwezeshaji.
Muwezeshaji wa Mafunzo ya kuibua habari za Uchunguzi Bi Edda Sanga, akisisitiza jambo jinsi ya kuibua habari za uchunguzi kwa waandishi wa habari wa Redio na TV wakati wa mkutano huo uliowashirikisha Waandishi wa habari wa Zanzibar. yaliofanyika katika hoteli ya Mazsons Shangani Zanzibar.
Waandishi wa habari wakiwa makini kufuatilia mafunzo hayo yaliokuwa yakitolewa na wawezeshaji kutoka Mfuko wa Vyombovya Habari Tanzania TMF.
Muwezeshaji Ndg. Ndimara Tegambwage, Mshauri wa Taaluma ya Habari Tanzania akitowa mada ya kuhusiana na habari za Uchunguzi kwa Waandishi wa habari wa Zanzibar ili kuweza kufaidika na Mfuko wa TMF kutumia fursa hiyo.
Waandishi wakiwa makini kufuatilia Mafunzo hayo yakitolewa na Wakufunzi kutoka Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania ili kuwawezesha kutumia fursa ya kupata ruzuku katika kutafuka habari za Uchunguzi Zanzibar.
Bi Edda Sanga akimsikiliza Mwandishi wa habari Ramadhani akitowa Wazolake kuhusiana na habari anazotaka kutayarisha wakati wa mafunzo hayo. waliofanyiwa ili kuweza kupata ruzuku kupitia mfuko huo wa TMF.
Muwezeshaji Ndg Ndimara akichukua Wao la mwandishi wa habari ili kuweza kupata Ruzuku kwa ajili yakufanya kazi za habari za uchunguzi Zanzibar.
No comments:
Post a Comment