Vijana wakipata joto ya jiwe baada ya kukutwa mchana wa Ramadhaan Machomanne Chake Pemba wakifanya mambo kinyume na maadili ya mwezi mtukufu.( Picha kwa hisani ya Abdi Suleiman, Pemba)
Elimu bado inahitajika kwa waumini kuweza kufahamu na kuelimishwa kuhusiana na funga kwani licha ya kuwa ni amri kutoka kwa Allaah Subhaanahu Wata'ala pia ni moja katika nguzo kuu tano za dini yetu ya kiislamu.
Kula kwa makusudi au kufanya jambo litakalobatilisha funga kwa makusudi mchana wa Ramadhaan si kwamba kunabatilisha funga tu bali kunaweza kukutoa katika dini pia kwa mujibu wa baadhi ya Maulamaa kwa kuikana moja katika nguzo za kiislamu.
Tusichoke kuwakumbusha ndugu zetu umuhimu wa kujitambua na kujielewa kwamba ni Waislamu kwanza na tutaulizwa na Muumba siku ya siku
Hata kama wamekula mchana hutakiwi kuchukua sheria mikononi kwako.Huyu bwana anaewapiga hawa vijana anatakiwa kuchukuliwa hatua kali kwa kuizalilisha dini ya kiislamu.Kama na yeye akikutwa kwenye dhinaa zake atakubali kupigwa mawe mia?
ReplyDeleteje wahusika wa mtandao huu zanzinews.com wanaridhia kupigwa kwa vijana hao? Lourence 0777458302
ReplyDeleteKumpiga mtu kwa makusudi kunatengua saumu.Sasa hawa wote wana makosa ya kujibu.
ReplyDelete