Na Mwandishi wetu
IDARA ya Uhamiaji itabadilisha tena hati za kusafiria kutokana
na kuwepo kwa matumizi mabaya yanayofanywa na baadhi ya wananchi.
Akizungumza
kwenye banda la uhamiaji katika viwanja vya maonesho ya 38 ya kimataifa ya
biashara ya sabasaba yanayofanyika Dar
es Salaam, Ofisa Uhusiano wa idara hiyo, Tatu Buruhani, alisema hatua hiyo
imefikiwa baada ya kubainika wananchi wengi wanafanya udanganyifu.
Alisema, wananchi wengi wamekuwa wakiwatumia
mawakala maarufu kama vishoka wa idara hiyo
kwa nia ya kupatiwa huduma hiyo kwa haraka na hivyo kuwasababishia wengi wao
kutapeliwa ikiwa ni pamoja na kubadilishiwa vyeti vyao.
“Kinachotokea hapa ni kwamba, mwingine
anachukua ile pasipoti anakwenda kuweka rehani, mwingine anauza, halafu anakuja
kukwambia kwamba imeibiwa. Katika uchunguzi tuliofanya tumebaini kuwa haziibiwi
bali wanazitumia vibaya pasipo kutambua umuhimu wake,” alisema.
Alisema utaratibu wa kubadilisha hati za
kusafiria ulianza mwaka 1961 kutokana na
changamoto kama na mabadiliko mengine
yalifanywa mwaka 1992 na ya mwisho kufanywa ilikuwa mwaka 2005.
No comments:
Post a Comment