Habari za Punde

Yanga yaifunga Timu ya Shangani katika Mchezo wa Kirafiki Uliofanyika Uwanja wa Amaan. Yainga imeshinda 2--0

Jopo la waamuzi likiongozwa na Muamuzi Mkongwe Issa Ahmada, wakiingia uwanjani kuchezesha mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Shangani ya Zanzibar. 
             Vikosi vya Yanga na Shangani wakiingia Uwanjani kukipiga katika mchezo wa kirafiki
Wachezaji wa timu ya Shangani wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Yanga kabla ya kuaza kwa mchezo huo uliofanyika uwanja wa Amaan timu ya Yanga imeshinda 2--0
Kikosi cha timu ya Shangani kilichopanda Ligi Daraja la Pili Taifa kilichopambana na Yanga katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan jioni hiyo na kukubali kufungwa kwa mabao 2--0. 
Kikosi cha timu ya Yanga kinachojiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom, kilichopambana na Timu ya Shangani ya Zanzibar na kutoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2--0.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga Haruna Niyonzima akiwapita mabeki wa timu ya Shangani katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.














Mshambuliaji wa Yanga Jaja akijiandaa kuzuiya mpira kifuani wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya Shangani iliofanyika uwanja wa Amaan Yanga imeshinda 2--0 
Kocha Mkuu wa Yanga Maximo na msaidizi wake wakifuatilia mchezo wao wa kujipima nguvu na timu ya Shangani ya Zanzibar mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan, timu ya Yanga imeshinda 2--0.
Mashabiki wa timu ya Yanga wakishangilia timu yao wakati ikicheza na timu ya Shangani katika uwanja wa Amaan.
Mchezaji wa timu ya Yanga Saimon Msuya akimpita beki wa timu ya Shangani Khamis Bakari, wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan.
Kiongozi wa timu ya Simba Kaburu akizungumza na Kiongozi wa Simba Zanzibar wakiwa katika jukwaa la VIP Amaan, wakati wa mchezo wa kirafii kati ya Yanga na Shangani.
Kocha Mkuu wa timu ya Simba Phiri akifuatilia mchezo wa kirafiki wa timu ya Yanga na Shangani uliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar.Timu ya Yanga imeshinda 2--0.
Kocha Mkuu wa timu ya Yanga Maximo akizungumza na wachezaji wake wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza.Yanga ikiwa mbele kwa baonmoja lililofungwa na Countinho.  
Mshambuliaji wa timu ya Shangani Hashim Haroun, akimpita beki wa timu ya Yanga Khamis Kiiza, wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan.
                                        Mshabiki wa timu ya Yanga akishangilia timu yake.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.