Na Maryam Salum,Pemba
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma
Majid Abdalla, amewataka viongozi wa taasisi
zilizo chini ya ofisi yake,kutoa ushirikiano wa hali ya juu, ili aweze
kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Alisema hayo wakati akizungumza na wananchi, wafanyakazi, masheha,pamoja
na viongozi wengine walio hudhuria katika hafla ya kumkabidhi majukumu ya uongozi Mkuu mpya wa wilaya
Chake Chake, Hanuna Ibrahim Massoud,kufuatia mabadiliko yaliofanywa na Rais wa
Zanzibar hivi karibuni.
Alisema bila ya kuwepo ushirikiano
kati ya wananchi na viongozi, mafanikio katika kazi zao hayatafikiwa.
Alisema iwapo wananchi watakuwa
karibu na viongozi na kutoa ushirikiano wa dhati kwa viongozi, wilaya hiyo
itapata mafanikio makubwa.
Alisema mkoa wa kusini umepata
bahati kubwa ambapo mwanamke ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa kitendo ambacho
hakijawahi kufanywa kisiwani humo.
Alimtaka Mkuu wa wilaya mpya kuwashirikisha wananchi yakiwemo makundi
mbali mbali katika kazi muhimu kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya na shehia.
Kwa upande wake mkuu mpya wa
wilaya ya Chake Chake, Hanuna Ibrahim Massoud, alihimiza ushirikiano kutoka kwa
wasaidizi wake ili wilaya hiyo iendelee kupata maendeleo.
Mohammed Juma Khatib, Mwenyekiti
wa CUF Chake Chake, aliwataka Viongozi hao kumuhakikishia Rais kuwa wanawake
wanaweza kwa kufanya kazi nzuri bila ya kusimamiwa na wanaume.
No comments:
Post a Comment