



Waziri wa Habari,Utamaduni , Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk amepiga marufuku shughuli zote za upigaji wa disko katika eneo la Kiwengwa mpaka pale Serikali ya wilaya itapotoa maelekezo maalumu ya upigaji wa disko hilo kwa utaratibu unaofaa.
Agizo hilo amelitoa huko Kiwengwa Mkoa wa kaskazini “A”wilaya ya kaskazini B Unguja katika Ofisi ya umoja wa maendeleo wa kijiji cha kiwengwa wakati alipokuwa akifanya mazungumzo na wamiliki wa mabaa mikahawa,na kumbi na starehe juu ya kukithiri wa upigaji wa magoma kucha.
Amesema amelazimika kuzifunga shughuli zote za upigaji wa madisko usiku kutokana na kutokua na utaratibu mzuri wa upigaji ngoma hizo usiku hali ambayo inapelekea wageni wa kitalii na wenyeji kuchukia hali hiyo kwa kukosa usingizi na kusumbuliwa wagonjwa wenye shindikizo la damu.
Amesema hali hiyo haiwezekani kuona inaendelea katika hali kama hiyo kwani inapoteza muelekeo na mstakabali mwema wanchi na raia kwa ujumla.
“Nimepokea message ya kwamba watalii wamefika kusema wanaondoka na kutafutiwa sehemu nyengine wakapunzike kutokana na zogo kuwa jingi la madisko, hili hiliwezekani liendelee” alisema Waziri.
Aidha alisema haiwezekani kuona utamaduni wa burudani unavurugwa kitu ambacho ni kosa kufanya hivyo na kwenda kinyume na taratibuzao silka zao.
“Kuanzia leo napiga marufuku mpaka sheha wa shehia hii aridhie hata kama kuna kibali, kwani sheha yeye ndio anae jua hali za raia wake kuna wagonjwa, wenye maradhi ya kuhitaji kupumzika hatutaki kuona masuala yasio na utaratibu.”aliongeza Waziri.
“Mimi kazi yangu ni kuutangaza utalii na sio utalii uharibiwe, tufahamu kua ulalii Zanzibar ndio uchumi unao tegemewa kwa sasa kwa hivyo tuulinde,”aliongeza Waziri Said.
Hata hivyo waziri huyo alichukia vitendo vya uasharati vilivyo tapakaa katika kijiji hicho na kujenga mabaa karibu na nyumba za ibada kitu ambacho aliagiza kwa mkuu wa wilaya kuyafanyia kazi.
Nao wazazi wa kiwengwa Othumani Mnyanja na Mtumwa Rashidi walisema Kiwengwa hivi sasa imepoteza muelekeo kwani watoto wao wanaishia katika madisko na kukosa masomo kitu ambacho ni hatari kwao.
Aidha walisema kua watoto wao wakiwa na umri mdogo na kujishughulisha na masuala ya kimapenzi jambo linalowafanya kupotea na kuacha mila za kislamu.
Wakitaja maeneo yanayopigwa miziki na watoto wao kwenda ni pamoja na maeneo ya Kigorofani, Vishani wazalendo pub, Kamili View, Obama Baa na Kigorofani eneo la mafarasi.
Nae miliki wa ukumbi wa Disko wa PERUU B, Peruce Osward Buhoma akiulizwa swali na waziri kwanini anafanya mazogo usiku alikiri kwa kusema hufanya hivyo kwaajili ya kuvuta wateja na kufanya ushindani kila mmoja kwa ajili ya kusikika zaidi kuliko mwenziwe.
Bibi huyo na wenzake walisema wanaweza kujirekebisha lakini pawe na utaratibu wa kupiga madisko kwa zamu na utaratibu mzuri utakaowekwa na uongozi.
ADABU YAO NI KUNYANGANYWA LESENI TUU HAO WAVAMIAJI.... Mimi nashangaa Hoteli zote za Kitalii Kuanzia Mmiliki, Manager, na wafanyakazi hata wakusafisha ni Wakenya, Waburundi, Waganda na hao tunaosema ni Ndugu zetu Watanganyika... Hata Wapiga Disco teki ni Wageni tena wote Ni JAhova Witness.... Kwanini Wafanye ushenzi wakupiga Madisco usiku mzima na kuwakera wana Nchi ambao ndio wanaomiliki maeneo hayo?
ReplyDeleteHuku Ulaya Madisco yanapigwa katika mahoteli Once In a BlUe Moon ( Yaani Kukiwa na shuhuli hadi shuhuli na hawapigi usiku kucha wala hawatumii Spika zitakazo wauzi wageni wengine na wapita njia.)..... Lakini huko Kwetu hao wajamaa Wakizungu na Hao Makafiri wa Kikenya na Kibara wamekua wakifanya hivo makusudi kwasababu Serikali haina Macho.. Na Sefu Ali Iddi ndio anaewapa Vibali..
Huo Mtindo wa Madisco unafanywa huko Unguja tu na hakuna hoteli Nyengine kule Ulaya wanakofanya hivo.