Habari za Punde

Jambazi auawa, achomwa moto

Na Joseph Ngilisho, Arusha
JAMBAZI sugu anayetumia ushirikiana katika kufanikisha matukio ya uhalifu mkoani hapa, ameuawa kwa kuteketezwa kwa moto na wananchi wenye hasira kali huku hirizi tatu alizokuwa amejifunga kiunoni zikigoma kuungua.
Jambazi huyo alitambulika kwa jina la Devii mkazi wa Olisiva mjini Arusha.
Aliuawa baada ya kuvamia nyumba ya mkazi mmoja akipitia katika tundu dogo la dirisha.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo,Emanuel Mejooli ambaye alivamiwa nyumbani kwake na jambazi huyo ,tukio hilo limetokea saa 8.30 usiku wa kuamkia jana wakati  akiwa amelala na familia yake.
Alisema alisikia kishindo kikubwa na baada ya kutoka chumbani alimkuta jambazi huyo akiwa katika chumba cha watoto.
Alisema baada ya kumkatama na kumuhoji alijitetea kuwa aliingia ndani kwa lengo la kumfanyia ‘surprise’ halia ambayo ilimlazimu kuita watu na kuanza kumshambulia na baadae walimmwagia mafuta ya petroli na kumteketeza kwa moto.
Jambazi huyo amekuwa akijihusisha na matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.


1 comment:

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.