Na Kija Elias, Moshi
MBUNGE wa jimbo la Vunjo, Augustino
Mrema, amewataka viongozi wanaounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA),kuacha kueneza propaganda chafu dhidi yake kwa kujipitisha jimboni mwake na kuwalaghai wapiga kura kwamba yeye ameahidi
kuwaachia jimbo hilo.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati
akizungumza na vyombo vya habari katika mji mdogo wa Himo, wilayani Moshi
mkoani humo.
Alisema malengo ya Ukawa sio katiba mpya kama ambavyo wengi walitarajia isipokuwa ni uchaguzi wa
mwaka 2015.
Alisema tangu Ukawa watoke bungeni ,
wamekuwa wakienda kwa wananchi na ajenda
yao ya katiba wameiacha
badala yake wanazungumzia uchaguzi mkuu ujao.
Alisema baadhi yao wamediriki hata kuwaambia wananchi wa
jimbo la Vunjo kuwa Mrema hatagombea
tena ubunge jambo ambalo amelikanusha
vikali.
Alisema bungeni ndio mahali sahihi pa
kujadiliana namna ya kupata katiba mpya na sio kutoka na kwenda barabarani kama ambavyo Ukawa wamekuwa wakifanya.
Alisisitiza kuwa kinachotakiwa ni wajumbe wote kushiriki katika bunge maalum la
katiba na sio kukimbia kazi hiyo kwa sababu waliaminiwa na Watanzania.
No comments:
Post a Comment