Na Joseph Ngilisho, Arusha
POLISI wametumia nguvu kuwatawanya
wanafunzi Chuo Kikuu cha St. Joseph mjini hapa, waliofunga barabara ya kutokea
Arusha kwenda Singinda katika eneo la Kisongo, wakilalamikia mitaala.
Katika tukio hilo wanafunzi 23 wanashikiliwa na
wanaendelea kuhojiwa.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya kuanzia saa
2:30 hadi saa 5:55 mchana na kusababisha magari yanayotumia barabara hiyo
kushindwa kupita.
Kamanda wa Polisi Mkoani hapa,
Liberatus Sabas,
alithibitisha kukamatwa kwa wanafunzi hao na kusema wanaendelea kuwahoji.
Wanafunzi hao wa shahada ya kwanza na
Diploma wanalalamikia kufundishwa mitaala ya nje hasa kutoka India na
wanahofu kwamba wanaweza kukosa ajira baada ya kumaliza.
Mgomo wa wanafunzi hao umedumu kwa wiki
moja sasa.
No comments:
Post a Comment