Habari za Punde

Shirika la Umeme Zanzibar ZECO likiwa katika Zoezi la Kuuza Umeme kupitia Mtandao wa ZANTEL

Wakala wa Kampuni ya Simu ya mkononi ya Zantel akitowa maelezo kwa Mtejawa ZECO aliyefika katika Ofisi za Zeco Gulioni kupata huduma ya kununua umeme, akipata maelezo jinsi ya kujiunga na mtandao wa EnzPesa kupata huduma ya kununua umeme kupitia katika simu yake.Zoezi hilo limeanza kwa majaribio kutowa huduma hiyo.kwa wateja wake.  

1 comment:

  1. Alhamdulilah Zeco sasa mutaacha kutuibia, au mtakuja na njia nyengine ya kuibia masikini za mungu?, mana mimi mushaniibia sana tu nikitia umeme alfu 20 naweza kutumia miezi mitatu nawasha taa 2 tu sipiki wala sina mke, sasa inakuaje nikija kutia umeme munanikata? kwasababu sijatia siku nyingi umeme tena munakata sana natia alfu 25 munanipa unit 5 tu si dhulma hii munoifanya? na ndugu muandishi tunaomba hili suala ukatuulizie kunakohusika, pengine hao wakubwa ata hawajui. inatakiwa umeme mtu atie kutokana na matumizi yake sio siku ngapi.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.