Na Anna Nkinda,Maelezo
TAKWIMU zinaonesha idadi ya
watoto wanaotumikishwa duniani inafikia milioni 169 kati ya hao wapo wenye umri
wa miaka mitano, wanaotoka katika familia maskini ambao hulazimika kufanya kazi ili waweze kuishi na
hivyo kukoa fursa ya upata elimu na malezi bora.
Kwa upande wa Tanzania asilimia
27.5 ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 17 wanatumikishwa katika ajira
hatarishi zikiwemo za kufanya kazi majumbani, sehemu za starehe, uvuvi,
migodini, mashamba ya tumbaku na machungwa.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na
mke wa Rais Kikwete, mama Salma Kikwete, wakati wa hafla ya chakula cha jioni
kilichoandaliwa kwa ajili ya kampeni ya kupambana na utumikishwaji wa
watoto iliyoandaliwa na International
Rescue Committee (IRC) katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mama Salma ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), alisema utumikishwaji
wa mtoto ni hali inayomkosesha
mtoto haki zake za msingi kama vile
elimu, afya, malezi na kutopata nafasi ya kucheza na watoto wenzake.
“Utumikishwaji wa mtoto una madhara
makubwa kwa mtoto mwenyewe, familia, jamii na taifa kwa ujumla. Kitendo hiki
humsababishia mtoto kuathirika kiakili,kiafya kisaikolojia,kimakuzi na hata
katika mazingira mengine hupelekea kifo chake,” alisema.
Pia husababisha umaskini kati
ya kizazi hadi kizazi, na hivyo kudidimiza maendeleo ya taifa.
Aidha alisema mtoto
anayetumikishwa hukosa ndoto za maisha
bora kwa siku za usoni kwa kuwa alikosa fursa hiyo akiwa mdogo.
Alisema mazingira mazuri ya
kisera na kisheria yametayarishwa kwa ajili ya kuwalinda watoto dhidi ya
unyanyasaji ukiwemo utumikishwaji katika ajira hatarishi na kinachotakiwa ni
juhudi za pamoja ili kuhakikisha watoto hawatumikishwi.
Mkurugenzi wa IRC Tanzania,
Elijah Okeyo, alisema ili kukabiliana na tatizo la ajira za watoto mwishoni mwa
mwaka 2012 Serikali ya Marekani kupitia Idara ya Kazi iliwapatia dola milioni 10 kwa ajii ya mradi wa WEKEZA
unaofanya kazi zake katika wilaya sita zilizopo mikoa ya Tanga na Kigoma.
Kupitia mradi huo, watoto
15,000 walitoka katika ajira hizo,
walilindwa ili wasiweze kujihusisha na ajira za watoto na kuweza kurudi skuli kuendelea na masomo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
IRC wa kanda ya Afrika ya Mashariki na pembe ya Afrika, Kurt Tjossem, alisema
kazi ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ni ya kila mtu
na siyo ya mtu mmoja hivyo wadau wote wa watoto waendelee kuwekeza katika elimu
kwani ndiyo ukombozi wa maisha yao.
Alisema inasikitisha kuona
mtoto anaacha skuli na kwenda kufanya kazi ili aweze kuongeza kipato cha
familia hali.
No comments:
Post a Comment