Habari za Punde

Mchezo wa Ligi Kuu Mafunzo na Mtende.

Kikosi cha timu ya Mtende kinachoshiriki Ligi Kuu ya Grand Malt, kilichokubali kipigo cha bao moja dhidi ya timu ya Mafunzo katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kikosi cha timu ya Mafunzo kilichotoa dozi kwa timu ya Mtende katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika uwanja wa amaan na kutoka na ushindi wa bao 1--0 
Mchezaji wa timu ya Mtende Suleiman Juma akijiandaa kumpita beki wa timu ya Mafunzo Mwalim Abdalla katika mchezo wa ligi kuu ya grand malt uliofanyika uwanja wa amaan, timu ya Mafunzo imeshinda.1-=-0.
Mchezaji wa timu ya Mtende Suleiman Juma, akiondoa mpira golini kwake huku mchezaji wa timu ya Mafunzo akijiandaa kumzuiya.
Mchezaji wa timu ya Mafunzo na Mtende wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya grand malt uliofanyika uwanja wa amaan, timu ya Mafunzo imeshinda 1--0. 

Mpenzi wa michezo Zanzibar na muamuzi wa mchezo wa mpira wakati ule na kuwahi kogombea nafasi ya Mwenyekiti wa ZFA Taifa akiwa katika uwanja wa amaan akijiandaa kufuatilia mchezo kati ya Mtende na Mafunzo.
Mchezaji wa timu ya Mafunzo akimpita beki wa timu ya Mtende katika mchezo wa ligi kuu ya grand malt uliofanyika uwanja wa amaan timu ya Mafunzo imeshinda 1-0.
                                          Wachezaji wakiwania mpira ukiwa hewani




Beki wa timu ya Mtende akiokoa mpira galini kwake wakatin wa mchezo wao na timu ya Mafunzo.timu ya mafunzo imeshinda 1--0
Viongozi na wachezaji wa timu ya Mtende wakiwa na majonzi baada ya timu yao ikiwa nyuma ya bao moja katika mchezo huo wao wa kwanza wa ligi kuu ya grand malt. 

Mshambuliaji wa timu ya Mafunzo akiwapita mabeki wa timu ya Mtende katika mchezo wa Ligi Kuu ya Grand Malt, uliofanyika uwanja wa amaan. 
Kocha wa timu yac Mtende akitowa maelekezo kwa wachezaji wake katika dakika za mwisho wa mchezo huo uliofanyika uwanja wa amaan.

1 comment:

  1. jamani mbona timu zote zina grand malt au sisi hatufati sheria za FIFA?, si fifa inasema timu zikicheza haziwezi kuwa na sponsor mmoja au mimi nimefahamu vibaya?, naomba muongozo

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.