Habari za Punde

Dk. Shein Awaapisha Wakuu wa Wilaya Pemba.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
       Zanzibar                                                                                                                                  30.9.2014
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Wakuu wa Wilaya pamoja na Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma.

Wakuu wa Wilaya walioapishwa na Dk. Shein ni Bwana Jabu Khamis Mbwana ambaye ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba.

Wengine ni Bwana Amran Masoud Amran ambaye ameapishwa kuwa Mkuu wa Wialaya ya Wete Pemba, Bwana Hemed Suleiman Abdalla ambaye  ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Pemba, pamoja na Bibi SSP Sida Mohamed Himid, aliyeapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja.

Aidha, Dk. Shein amemuapisha Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma kuendelea na nyadhifa zao kwa kipindi chengine cha miaka mitatu ambapo Bwana Mohammed Fakih Mohammed ameapishwa kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma.

Wengine ambao  wameapishwa kuwa Wajumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma ni Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar  Hamid Mahmoud Hamid, Bwana Ali Rajab Juma, Balozi Hussein Said Khatib, Bwana Issa Mohammed Suleiman pamoja na Bwana Mabrouk Jabu Makame.

Hafla hiyo, ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali,Washauri wa Rais wa Zanzibar, Wakuu wa Vikosi Maalum vya SMZ  na viongozi wengine wa Serikali


Uteuzi wa viongozi hao umeanza jana tarehe 29 Septemba 2014.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.