Na Madina Issa
MBUZI 120 wamekamatwa maeneo ya
pwani ya Kizingo baada ya kupitishwa katika bandari bubu isiyoruhusika
kisheria.
Mbuzi hao hivi sasa
wamekabidhiwa Udara ya Mifugo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kujulikana kama
wapo salama.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi ofisini kwake Muembemadema, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi,
Mkadam Khamis Mkadam, alisema tukio hilo lilitokea Septemba 27 majira ya saa
3:00 usiku katika bahari ya Kizingo wilaya ya majini Unguja.
Alisema watu hao walikamatwa
wakati wakiwashusha mbuzi hao katika bandari hiyo kwa madai boti yao waliyokuwa
wamepakia imeharibika na ndipo walipoona washushie maeneo hayo.
Aliyataja matukio mengine ni
kuchomwa kisu na kupigwa mapanga vijana
wawili ambapo mmoja ni mkaazi wa Mwembeshauri na mwengine ni mkazi wa Amani
wilaya ya mjini Unguja.
Alisema tukio la kupigwa kisu
kijana Jamali Abdallah Mohammed (18) limetokea Septemba 25 mwaka huu majira ya
3:30 Mwembeshauri na kujeruhiwa katika sehemu zake za siri ambapo mtuhumiwa
alitambuliwa kwa jina la Munawir Abdulla mkaazi wa Muembeshauri.
Alisema kijana huyo alifikishwa
hospitala ya Mnazimmoja kwa matibabu zaidi na hali yake inaendelea vizuri huku
jeshi la polisi linaendelea na upelelezi juu ya tukio hilo.
Tukio jengine lilitokea
Septemba 24 saa 1:00 usiku Miembeni ambapo Omar Yasir Juma (18) mkaazi wa Amani
alishambuliwa na watu wawili ambao hawakufahamika kwa kupigwa panga sehemu ya kichwa na mdomoni
pamoja na kunyang’anywa simu nne aina ya Nokia na fedha taslimu shilingi 15,000
pamoja na vocha za Zantel zenye thamani ya shilingi 60,000.
Aliwataka wananchi kuwa
waangalifu na kufuata sheria bila ya kushurutishwa.
No comments:
Post a Comment