Na Fatina Mathias, Dodoma
Kituo cha Demokrasia Tanzania
(TCD) kinachoundwa na vyama vya siasa, kimekubali mjadala wa Bunge la Katiba
uendelee hadi Oktoba 4, ndipo Bunge hilo liahirishwe.
Tamko hilo lilitolewa jana na
Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo wakati akizungumza na waandishi wa habari bungeni
mjini Dodoma.
Alisema bunge hilo kwa sasa
linafanya kazi kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 254 lililotolewa na Rais
Jakaya Kikwete.
“Kwa mujibu wa sheria ya
mabadiliko ya katiba baada ya bunge hilo kumaliza kutunga katiba,ingefuata
hatua ya kura ya maoni kuthibitisha katiba hatua ambayo italazimisha uchaguzi
mkuu wa 2015 kuahirishwa, hivyo tumeona
ni kheri mchakato uahirishwe na uendelee baada ya uchaguzi mkuu wa
mwakani,”alisema.
Alisema pamoja na kazi
inayofanywa na bunge hilo, lakini haliwezi utoa katiba mpya itakayotumika
katika uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa muda hautoshi kukamilisha kazi hiyo.
Aidha alisema kwa mujibu wa
sheria ya mabadiliko ya katiba mwisho wa mchakato ni kura ya maoni
itakayofanyika mwezi Aprili mwakani na kama itabidi kurudiwa kwa mujibu wa
sheria iliyotajwa itabidi irudiwe mwezi Juni au Julai 2015 muda ambao bunge la
Jamhuri linatakiwa livunjwe kwa ajili ya uchaguzi mkuu, hivyo ili katiba mpya
itumike kwenye uchaguzi inabidi uhai wa bunge uongezwe zaidi ya 2015 jambo
ambalo hawaliungi mkono.
Alisema kwa sasa inabidi
matayarisho kwa ajili ya uchaguzi wa vijiji,vitongoji na mitaa yaanze haraka
iwezekanavyo kwa serikali kuchukua hatua za kisheria ili uchaguzi ufanyike
mapema mwakani.
“Kwamba kwa vile uchaguzi mkuu
utafanyika kwa kutumia katiba ya Jamhuri ya mwaka 1977 ni muhimu kufanya
mabadiliko kidogo katika katiba pamoja na sheria ya uchaguzi itakayowezesha
nchi kufanya uchaguzi huru na wa haki,”alisema.
Alitaja mambo ambayo wameyakubali
kuwa ni kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi
ambayo itasimamia uchaguzi na mshindi wa
uchaguzi wa rais ashinde kwa zaidi ya
asilimia 50.
Alisema viongozi wakuu wa vyama
wanaounda TCD wamempongeza Rais Kikwete kwa ujasiri wake na imani yake katika
kuimarisha demokrasia nchini wa kuanzisha mchakato wa kuandika katiba ya nchi.
Aidha walimpongeza Rais kwa
kukubali kukutana na kushauriana kuhusu mambo ya muhimu kwa mustakabali wa
Taifa kwa lengo la kudumisha amani,upendo na mshikamano.
Vyama vinavyounda TCD ni CCM, CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI, TLP, UDP
ambavyo vina wawakilishi bungeni na UPDP kinachowakilisha vyama visivyo na
wabunge bungeni.
ccm sasa mumekwisha 2015 lazima mutoke kwanza munatutesea mashekhe wetu, ndo kabisaaa munatutia ghadhab
ReplyDeleteccm 2015 mimi sikupigieni kura, sabu nikikupeni kura yangu nitakuwa nashangiria mambo yote wanayofanyiwa ndugu zetu katika Uisilamu, nyinyi ndio sababu ya yote haya na bado munafurahiya.
ReplyDeleteKutopatikana kwa katiba mpya ni mbinu za CCM ili itawale kwa miaka mitano zaidi. Kweli CCM ni jabali lisilo tetereka. CCM juu,juu ,juu zaidi.
ReplyDelete