Na Bakar Mussa, Pemba
Lita 250 za mafuta zenye
thamani ya shilingi milioni tano, zimekamatwa na vikosi vya SMZ katika bandari
ya Uchungani Wesha mkoa wa kusini Pemba.
Akizungumza na waandishi wa habari,Msaidizi
Kamishna wa Zimamoto, Iddi Khamis Juma, alisema vikosi hivyo vikiwa katika kazi zake za kawaida
vilifanikiwa kukamata mafuta hayo majira ya saa 10:30 asubuhi ya kuamkia jana.
Alisema askari hao walikamata mafuta
hayo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema na kwa bahati mbaya
hawakufanikiwa kuwakamata wahusika.
Alisema kikosi hicho kilichopo
Mkumbuu, kimekuwa na kawaida ya kufanya doria kila pembe ya bahari, ambapo hivi
karibuni walifanikiwa kukamata shehena ya mbao ambazo ziliingizwa kinyume na
utaratibu na kuzifikisha mamlaka husika kwa hatua za kisheria.
Aliwapongeza wapiganaji hao kwa
moyo wao wa kishujaa na wa kizalendo licha ya changamoto mbali mbali
zinazowakabili.
No comments:
Post a Comment