Na Kija Elias, Moshi
Wakati serikali ikihaha
kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu, katika hali ya kusikitisha, mwalimu wa
skuli ya sekondari ya Muungano, Rashid Ndoile (30) anashilikiwa na polisi
mkoani Kilimanjaro, kwa tuhuma za kufumaniwa akifanya ngono na mwanafunzi gesti
moja iliyopo mji mdogo wa Himo.
Tukio hilo la kusikitisha ambalo
limethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Koka Moita,
lilitokea Oktoba 3 saa tano asubuhi, katika nyuma ya kulala wageni ijulikanayo
kwa jina la Kilimanjaro.
Alisema wawili hao walifumaniwa
na wazazi wa mwanafunzi.
Alisema siku ya tukio mwalimu
huyo alionekana na wazazi wa mwanafunzi huyo, akipita na pikipiki huku akiwa
amembeba mwanafunzi huyo, hali ambayo iliibua mashaka na kuamua kumfuatilia.
Alisema baada ya wazazi
kumfuatilia mwalimu huyo, waliwakuta
chumbani katika gesti hiyo jambo ambalo
liliwafanya watoe taarifa polisi na mwalimu huyo kukamatwa.
Alisema kwa sasa, mwalimu huyo
anashikiliwa kituo cha polisi Himo kwa mahojiano zaidi na kwamba upelelezi
utakapokamilika, atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.
Wakati huo huo, mwalimu mmoja wa skuli ya sekondari ya Uparo,
aliyefahamika kwa jina moja la Matanda,anadaiwa kufumaniwa na wanafunzi wa skuli
ya msingi iliyopo jirani na skuli anayofundisha akifanya ngono na mwanafunzi
wake wa kidato cha tatu katika kichaka karibu na skuli hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
baadhi ya wazazi wenye wanafunzi wanaosoma katika skuli hiyo iliyopo
halmashauri ya wilaya ya Moshi Vijijini, mara baada ya kufumaniwa, tukio hilo lilimalizwa
kimya kimya na mkuu wa skuli hiyo ambapo baadaye mwalimu huyo alihamishiwa skuli
ya sekondari ya Langasani iliyopo eneo la TPC.
Ofisa Elimu wa sekondari
halmashauri ya wilaya ya Moshi Vijijini, Dk. George Jidamva, alipoulizwa
kuhusiana na tuhuma hizo alikana kuzifahamu na kuahidi kufuatilia.
No comments:
Post a Comment