Na Mwanajuma Mmanga
Jumla ya watoto 81 wamezaliwa
katika mkesha wa sikukuu ya Idd el Hajj katika hospitali ya Mnanzimmoja na Muembeladu.
Kati ya watoto hao, 61
wamezaliwa hospitali ya Mnazimmoja wakiwemo wanawake wakiwa 34, ambapo wawili
walifariki dunia baada ya kuzaliwa wakati mama zao wakiwa njia kuelekea hospitali kwa ajili
ya kujifungua.
Katika hospitali ya Muembeladu walozaliwa
watoto 20 katika ya hao wanawake 8 na wanaume 12.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi, Katibu wa hospitali ya Mnazimmoja, Hassan Makame, alisema watoto
hao walizaliwa wakiwa na uzito wa juu ni kilo 3.5 na uzito wa chini ni kilo 2.
Alisema watoto hao wako salama
na hawana matatizo yoyote ya kiafya na kwamba wameruhusiwa kurudi nyumbani.
Msaidizi Muuguzi Dhamana wa hospitali
ya Muembeladu, Mgret Sylveter Tayari, alisema uzito wa watoto waliozaliwa hospitali
hiyo ni baina ya kilo 4.2 na 3.
Akizitaja changamoto wanazokumbana
nazo katika kuwahudumia mama wajawazito wakati wanapofika kituoni kujifungua ni
pamoja na kuchelewa kufika hospitali wakisubiri waumwe na uchungu.
Aidha, alisema wengine
wanatumia dawa za asili kuongeza uchungu hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha
yao na watoto.
Aliitaka jamii kuhamasika
kuvitumia vituo vya afya na hospitali kwa ajili ya kupata matibabu.
No comments:
Post a Comment