Na Mwandishi wetu
Chama cha Wanahabari Wanawake
Tanzania (TAMWA) leo kitazindua taarifa
ya utafiti kuhusu kiwango cha unywaji
pombe na ukatili wa kijinsia.
Taarifa ya utafiti huo inaonesha kiwango cha unywaji pombe, sababu
zinazopelekea watu kunywa kupita kiasi, madhara, kiwango cha upatikanaji pombe,
ufahamu kuhusu matumizi na uhusiano kati ya matumizi ya pombe na ukatili wa
kijinsia katika wilaya ya Kinondoni.
Kuna uhusiano mkubwa kati ya
matumizi ya pombe na tabia ya kufanya vurugu, ambapo kwa mujibu wa taarifa ya
Utafiti wa Afya na Idadi ya Watu Tanzania (TDHS) ya mwaka 2010, matokeo
yalionesha wanawake ambao waume zao ni walevi wako katika hatari ya kufikwa na
ukatili wa kihisia, kimwili au kingono mara mbili zaidi ya wanawake ambao waume
wao hawanywi pombe.
Uzinduzi wa utafiti huo ni
sehemu ya mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia unaotokana na matumizi ya
pombe dhidi ya wanawake na wasichana, unaofadhiliwa na Taasisi ya Kimataifa ya
IOGT wenye lengo la kujenga uelewa miongoni mwa jamii juu ya madhara yatokanayo
na pombe ili kupambana na ukatili unaotokana na pombe.
Mradi wa IOGT una miaka mitatu
ya mafanikio tangu umefanya kazi na TAMWA.
No comments:
Post a Comment