Habari za Punde

Zanzibar Yazindua Chanjo ya Surua na Rubella

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Jamala Adam Taib akielezea utaratibu wa kampeni ya chanjo ya Surua na Rubela pamoja na matone ya Vitamin A na dawa za minyoo itakavyoendeshwa katika uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo  kitaifa uliofanyika kijiji cha Uroa Mkoa wa Kusini Unguja.
Wazazi na wanafunzi  wa kijiji cha Uroa waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya Surua na Rubela wakimsikiliza mgeni rasmi katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani) kabla ya uzinduzi wa Chanjo hizo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya Surua na Rubella Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimpatia mtoto matone ya Vitamine A katika uzinduzi wa chanjo hiyo kitaifa uliofanyika  kijiji cha Uroa.

Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Uroa akimpatia mtoto chanjo ya surua na Rubella kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika kijijini hapo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.