Habari za Punde

Ziara ya Ujumbe wa Kilindi Kisiwani Pemba.

Afisa Mdhamini Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Pemba,Ndg.Saleh Mbarouk Omar akizungumza na ujumbe wa watendaji kumi kutoka mkoani Tanga, ukiongozwa na mkuu wa

wilaya ya Kilindi Suleima Salim (kulia) wakati ujumbe huo ulipofika kisiwani humo kwa ziara ya kujifunza (picha na Haji Nassor, Pemba)

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga Ndg.Suleiman Salim akitoa neno la shukuran kwa uongozi wa mkoa wa kusini Pemba, mara ujumbe huo kutoka Tanga ulipowasili kisiwani humo kwa ziara ya kikazi baina na halmashauri , mabaraza ya miji ya Tanga na mko wa kusini Pemba.
Mkuu wa Wilaya ya Chakechake,Bi.Hanuna Ibrahim Masoud akitoa taarifa fupi ya wilaya yake kiujumla, kwa ujumbe wa watendaji kumi kutoka mkoani Tanga, ukiongozwa na mkuu wa wilaya ya Kilindi Ndg.Suleima Salim,  wakati ujumbe huo ulipofika kisiwani humo kwa ziara ya kujifunza.

Katibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chakechake Pemba,Ndg.Hassan Abdalla Rashid, akitoa maelezo mafupi kwa ujumbe wa watu kumi kutoka mkoa wa Tanga, wakati ujumbe huo ulipotembelea bandari ya Wesha, kabla ya kuanza ziara rasmi kisiwani Pemba, kuangalia namna halimashauri na mabaraza ya miji Pemba anavyofanya kazi zake
Ujumbe wa watu kumi kutoka mkoa wa Tanga, ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, ukitembelea bandari ya Wesha wilaya ya Chakechake, kabla ya kuanza ziara rasmi kisiwani Pemba, kuangalia namna halimashauri na mabaraza ya miji Pemba yanavyofanya kazi zake (Picha na Haji Nassor, Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.