Na Kija Elias, Moshi
Imeelezwa uwepo wa fedha nyingi
bandia nchini umechangia kupunguza thamani ya fedha halisi na kusababisha
mfumuko wa bei.
Hayo yaliemwa na Mkurugenzi wa
Benki Kuu ya Tanzania tawi la Arusha,Said Chiguma, wakati wa kikao cha dharura cha Kamati ya
Ushauri ya mkoa wa Kilimanjaro (RCC),ambapo alisema nchi inakabiliwa na tatizo
kubwa la uingizwaji wa fedha bandia
jambo, ambalo limesababisha
baadhi ya fedha hizo kuingizwa kwenye mzunguko huo.
Alisema miongoni mwa mikoa
iliyoathirika na uwepo wa fedha hizo ni pamoja na Arusha ambao unaongoza kwa
kuwa na idadi kubwa ya noti bandia za shilingi 10,000 kwa kuwa na jumla ya noti bandia 102 na noti za shilingi 5,000 kwa
kipindi cha Julai 2013 hadi Juni 2014.
Alisema mkoa ambao unafuatia ni Manyara ambao una
noti za shilingi 10,000 zinazofikia 84.
Alitoa rai kwa wananchi wa
kanda ya kaskazini kuwa makini pindi wanapopokea fedha hususani nyakati za
usiku.
Alisema takwimu hizo zinatokana
na matukio yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi ambapo kwa upande wa fedha
bandia zilizopatikana kutoka katika benki za biashara kwa mkoa wa Arusha
unaongoza kwa kuwa na jumla ya noti bandia 426 ambayo sawa na asilimia 55.9.
Mkurugenzi wa Benki ya Wananchi
Mwanga (MCB), Abi Mangia, alisema wakulima wanakabiliwa na changamoto ya
ukosefu wa elimu ya ujasiriamali wa kilimo hali ambayo imekuwa ikirudisha nyuma
jitihada za wakulima hao kujikwamua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment