Na Meibaku Mollel, TSJ Pemba
Uongozi wa kiwanda cha mafuta
ya makonyo na arki ya mimea kisiwani Pemba, unatarajia kuanza kuzalisha bidhaa
mbali mbali zenye ubora, kwa kushirkiana na kampuni ya Land ya Japan, kuanzia
mwezi Disemba mwaka huu, ikiwa ni pamoja na mishumaa.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hii ofisini kwake, Meneja wa kiwanda hicho, Ramadhani Kombo Ferouz, alisema
uzalishaji wa bidhaa hizo ambazo baadae zitawekwa nembo maalumu, umekuja kutokana
na kuendelea kuwepo ushirikiano na kampuni hiyo.
Alisema wameamua kuanzisha
ushirikiano wa kibiashara na kampuni hiyo, ili k kutengeneza bidhaa
zilizoongezewa ubora wa hali ya juu, ambazo zitakitangaza kiwanda hicho.
Alisema bidhaa wanazotarajia
kuzalisha mwezi ujao, zitauzwa ndani na nje ya Zanzibar na zitakuwa na nembo
yenye jina la Zanzibar Valore.
Alisema uzalishaji bado
haujanza isipokuwa wametengeneza baadhi ya vifaa kwa ajili ya kufanya maonesho
ya awali ya bidhaa wanazotarajia kuzalisha kwa ushirikiano na kampuni hiyo.
Alisema wataalamu kutoka Japan
watawasili Zanzibar mwanzoni mwa mwezi ujao kwa ajili matayarisho ya uzalishaji.
No comments:
Post a Comment