Na Augusta Njoji, Dodoma
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania,
zitafanya uchunguzi wa matukio ya kulenga shabaha katika eneo la Unguja Ukuu
yaliyofanywa na JWTZ Zanzibar kama
yamesabanisha madhara na ikibainika kuna
walioathirika watalipwa fidia.
Waziri wa wizara hiyo, Dk.
Hussein Mwinyi, alisema hayo jana bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Baraza
la Wawakilishi, Jaku Hashim Ayoub.
Katika swali lake Jaku alitaka
kujua kama serikali ipo tayari kutoa fidia kwa madhara yanayotokea na
yatakayotokea kwa wananchi wa Unguja Ukuu na wale ambao tayari wameathirika.
Pia alitaka kujua serikali ina
mpango gani wa kubadilisha matumizi ya eneo hilo haraka ili kunusuru uwezekano
wa kutokea vifo na majeruhi kwa wananchi
wa maeneo hayo.
Akijibu maswali hayo, Dk.
Mwinyi, alisema mazoezi ya kijeshi ndio msingi mkuu wa utendaji kivita katika
majeshi yote duniani likiwemo Jeshi la Ulinzi ka Wananchi wa Tanzania hivyo
hayana budi kufanyika.
Alisema kwa sasa jeshi halina
eneo mbadala la kufanyia mazoezi ya kijeshi kisiwani Unguja kwa kuwa hakuna
maeneo mengine makubwa yanayoweza kutumika kwa majukumu hayo.
No comments:
Post a Comment