Habari za Punde

MKUTANO WA MABALOZI NA WENYEVITI MASKANI WILAYA KUSINI UNGUJA.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipofika katika viwanja vya  Visitors Inn  Hotel Jambiani Wilaya ya Kusini Unguja alipofika leo kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia) Mwenyekiti wa Wilaya ya Kusini Unguja Abdul-Aziz Hamad Vuai wakiwa katika ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya ya Kusini Unguja katika mkutano maalum wa kuimarisha Chama kwa Mabalozi na Wenyeviti wa Wilaya hiyo
Wasoma  Utenzi Nezi Khamis na Amina Haji kutoka Jambiani wakihani utenzi wao wakati wa Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani  katika ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya ya Kusini akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkoa wa Kusini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Risala ya Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani  katika  ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya Kusini wakati wa Mkutano maalum wa kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkoa wa Kusini Unguja,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani  katika  ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya Kusini akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkoa wa Kusini Unguja 
Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani Wilaya ya Kusini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipookuwa akizungumza na Viongozi hao wa Mashina wa Jimbo la Muyuni katika ukumbi  wa Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya Kusini akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama Mkoa wa Kusini Unguja 
Mwenyekiti wa Wilaya ya Kusini Unguja Abdul-Aziz Hamad Vuai akionesha Ilani ya Chama kwa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani wakati wa Mkutano maalum wa kuimarisha Chama uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika Jimbo la Muyuni katika ukumbi  wa Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya Kusini, 
Balozi wa Shina namba 8 Jimbo la Makunduchi Tawi la Kizimkazi Dimbani Mwajuma Ramadhan Ali akitoa mchango wake mbele ya Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipofika kuzungumza na Mabalozi wa Wilaya ya Kusini Unguja leo katika ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Unguja akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkoa wa Kusini Unguja(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.