Habari za Punde

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO SAIDI ALI MBAROUK AKUTANA NA BALOZI WA UFARANSA OFISINI KWAKE KIKWAJUNI MJINI ZANZIBAR.

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bi. Malika Berak alipomtembelea Ofisini kwake Kikwajuni.
Ofisa  Ubalozi wa Ufaransa anaeshughulikia Ushirikiano na Utamaduni Philippe Boncour akisisitiza jambo katika mazungumzo na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk (hayupo pichani) Ofisini kwake Kikwajuni.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akimkabidhi zawadi ya kanga Balozi Malika baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Wizarani kwake Kikwajuni. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

1 comment:

  1. Mimi huwa najiuliza hivi hawa wenzetu huwa mabalozi kweli au ni wahuni tu. Hivi kweli mtu mwenye hadhi ya balozi anaonana na waziri au rais wa nchi anavaa kimini-skirt kweli??? Yuko almost uchi kabisaaaaa. Niliwahi kusikia nchi husika inaweza kumkataa balozi kuwakilisha nchini mwake ikiona kuna sababu za kufanya hivyo. Kama ni kweli nafikiri na hawa wengine ipo haja ya kuwakataa.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.