Habari za Punde

Balozi Seif Apokea Maandamano ya Kuipongeza Hutuba ya Rais Shein, Elimu Bila ya Malipo Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokea maandamano ya Wanafunzi na wazazi wa Wil;aya ya Magharibi kuunga mkono kauli ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein kufuta uchangiaji kwa elimu ya msingi na ada za mitihani kwa Kidatu cha Nne na Cha Sita aliyoitoa katika kilele cha sherehe za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi  ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapongeza Wazazi, walezi na Wanafunzi wa Wilaya ya Magharibi kwa uamuzi wao wa kupongeza Rais wa Zanzibar Dr. Shein kutokana  na kauli yake ya kufuta  uchangiaji wa elimu Nchini.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Ali Juma Shamhuna akitoa kauli ya kutolewa matokeo ya mitihani ya darasa la saba na Kidatu cha pili ijumaa ijayo hapo katika Mkutano wa kupongeza Rais wa Zanzibar kutoa kauli ya kufuta  uchagizji wa elimu Nchini.
Vijana na Wanafunzi wa Skuli za Wilaya ya Magharibi wakionyesha kuunga mkono kauli ya Dr. Shein kufuta uchangiaji kwa elimu maskulini.
Baadhi ya wazee na wazazi wa Wilaya ya Magharibi wakiwa katika mkutano wa Kumpongeza Rais Shein kufuta uchangiaji kwa elimu ya msingi na ada za mitihani kwa Kidatu cha Nne na Cha Sita hapo viwanja vya michezo nyuma ya Skuli ya Mwanakwerekwe “C “ (Picha na – OMPR )

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.