Michuano ya kuwania Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2015 linaendelea leo katika uwanja wa Amaan kwa mechi mbili za Nusu Fainal itakazozikutanisha timu za Polisi, Mtibwa, JKU na Simba.
Timu ya JKU imefanikiwa kuingia Nusu fainali ya Kombe hilo kwa kuitowa kwa tabu timu ya Yanga kwa bao 1--0 lililofungwa na msdhambuliaji wake Amour Janja katika kipindi cha pili cha mchezo huo katika dakika ya 67 ya mchezo huo uliofanyika uwanja wa Amaan.
Michezo hiyo ya Nusu Fainali inatarajiwa kutimua vumbi jioni hii kwa kuzikutanisha timu ya Mtibwa na JKU saa kumi jioni katika uwanja wa Amaan. kila timu ikiwania kuingia fainali ili kuwa bingwa kwa mwaka huu wa Kombe la Mapinduzi.
Mchezo wa usiku saa mbili utazikutanisha timu ya Polisi ya Zanzibar na Simba, mchezo huo unasubiriwa kwa hamu kuona na atatoka kifua mbele . Timu ya Polisi imeingia Nusu fainali kwa kuitoa timu ya KCC ya Uganda kwa njia ya penenti na kufanikiwa kuingia nusu fainal
Nayo timu ya Simba imefanikiwa kutinga Nusu fainal kwa kuifunga timu ya Taifa ya Jangombe (Wakombozi wa Ngambu) kwa kuwafunga mabao 4--0.
Tunazitakia kila la kheri timu zetu zinazishiriki Michuano ya Kombe la Mapinduzi leo jioni.
No comments:
Post a Comment