Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum, Mhe Haji Omary Kheri, akiwana Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mhe Issa Haji Gavu, na Mkurugenzi Mkuu wa Shiriki la Bandari Zanzibar Ndg. Abdalla Juma, wakiwasili katika bandari ya Zanzibar kwa ajili ya Uzinduzi wa Tagi Mpya ya Shirika la Mabdari Zanzibar ilionunuliwa kupitia Mkopo wa Masharti Nafuu uliotolewa na Benki ya Watu wa Zanzibar wa Euro 4.43 milioni sawa na 9.7 Bilioni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum. Mhe Haji Omary Kheri, akikata utepe kuashiria kwa kulizindua rasmin Tagi ya kisasa ya Shirika la Bandari Zanzibar kwa kutowa huduma mbalimbali za Uokozi na kuvutia meli, uzinduzi huo umefanyika katika bandari ya forodhani., kushoto Naibu Waziri wa Miundombuni na Mawasiliano Zanzibar Mhe Issa Haji Gavu na kulia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndg Abdalla Juma. wakati akizundua Tagi hiyo.
Tagi Mpya ya Shirika la Bandari Zanzibar ikiwa katika uzinduzi wake katika bahari ya forodhani baada ya kuzinduliwa.
Tagi Mpya ya Shirika la Mandari Zanzibar inayoitwa SHUWARI, ikionesha moja ya huduma inayotolewa na Tagi hiyo wakati wa chombo kinapotokea na ajali ya moto ikirusha maji baharini wakati wa uzinduzi wake uliofanyika katika bahari ya forodhani, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wageni waalikwa wakishuhudia Uzinduzi wa Tagi ya SHUWARI uliofanyika katika bandari ya abiria forodhani Zanzibar wakiangalia huduma za Tagi hiyo.
Waalikwa wa Uzinduzi wa Tagi mpya wakifuatilia uzinduzi huo na kuangalia moja ya huduma inayotolewa na Tagi hiyo wakati wa uzinduzi wake.
Mhe Waziri Omar Haji Kheri na Waziri wa Kilimo na Maliasili Mhe Dk. Sira Ubwa, wakishuka katika Tagi hiyo baada ya kuizundua na kuzunguka na kutowa huduma ya uokoaji kwa kumwaga maji kuonesha moja ya huduma za uzimaji moto ikitokea ajali ya moto kwa vyombo vya usafiri wa baharini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndg Abdallah Juma, akisoma risala ya mafanikio wakati wa Uzinduzi wa Tagi ya Shuwari katika Bandari ya Forodhani Zanzibar, ikiwa ni moja ya Shamrashamra za kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Bandari Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya Uzinduzi wa Tagi Mpya ya Shirika hilo uliofanyika katika viwanja vya bandari ya forodhani Zanzibar.
Waheshimiwa wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndg Abdallah Juma akitowa maelezo ya ununuzi wa Tagi hiyo mpya na kuishukuru Benki ya Watu wa Zanzibar(PBZ) kwa msaada wao wa Mkopo wa masharti nafuu kuweza kuinunua Tagi hiyo ili kuimarisha huduma katika Bandari ya Zanzibar kwa meli zinazitia naga katika Bandari ya Zanzibar.
Wafanyakazi wa Shirika la Bandari Zanzibar wakifuatila hafla ya Uzinduzi wa Tagi ya Shuwari iliozinduliwa katika Bandari ya Zanzibar ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar kilele chake kinafanyika 12 January 2015 katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
gati 4.4million euros.....huu ni wizi wa wazi wazi...waonyeshe invoices na transactions ya ununuzi...wizi wizi wizi....
ReplyDeleteNi tagi sio gati
Delete