Habari za Punde

Rais Mstaff Ali Hassan Mwinyi Ashiriki Matembezi ya Maadhimisho ya miaka 90 ya Skuli ya Ben Bella

 Rais Mstaaf wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, akiongoza Matembezi ya kilomita 5.7 kuadhimisha miaka 90 ya Skuli ya Sekondari ya Ben Bella, yaliowashirikisha Wanafunzi waliowahi kusoma Skuli hiyo na wanaoendelea kusoma,  
 Washiriki wa Matembezi ya Skuli ya BenBella wakiwa katika matembezi hayo katika barabara ya kinazini kuelekea kariakoo na kumalizia viwanja vya mnazi mmoja. 
 Wanafunzi wa Skuli ya Ben Bella wakishiriki katika matembezi hayo wakiwa na Ujumbe wa Kumuelimisha Mtoto wa Kike Umeelimisha Jamii Nzima Zanzibar.
 Wananchi na Vijana wa Kikundi cha Mazoezi cha Mwanakwerekwe wakishiriki katika matembezi hayo.
 Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Ben Bella wakiwa katika matembezi hayo wakiwa katika barabara ya kariakoo kuelekea viwanja vya mnazi mmoja kumalizia matembezi hayo yalioongozwa na Mzee Ruksa Ali Hassan Mwinyi. 
 Washiriki wa Matembezi hayo waliosoma Skuli hiyo wakishiriki matembezi hayo ya kilomita 5.7, yalioanzia Skuli ya Ben Bella na kumalizia viwanja vya mnazi mmoja

Rais Mstaaf Mhe Ali Hassan Mwinyi na Waziri wa Elimu wakimalizia matebezi hayo wakipiota mbele ya skuli ya Ben Bella na kuingia katika viwanja vya mnazi mmoja.












No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.