Habari za Punde

Shamrashamra za Kutimia Miaka 51 ya Mapinduzi Uzinduzi wa Miradi ya Maendeleo Pemba

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui, akiondoa kitambaa kuashiria uzinguzi wa kisima cha maji kilindi wilaya ya Chake Chake, katika shamra shamra za miaka 51 ya Mapinduzi
WAZIRI wa Biashara, Viwanda na masoko Zanzibar Mhe: Nassor Ahmed Mazrui, akipata maelezo ya kisima cha maji kilichochimbwa na ZAWA kwa ufadhili wa SMZ, kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa ZAWA Pemba Mhe:Juma Ali Othaman, kabla ya kukizindua rasm ikiwa ni shamra shamra za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui, akiwasha mashine ya maji kuashiria ufunguzi wa kisima cha kusukumia maji kilindi Chake Chake Pemba, kilichojengwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ikiwa ni shamra shamra za miaka 51 ya Mapinduzi
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui, akikizindua kwa maji kwa kufungua koki kwa kuzungusha kuashiria uzinduzi wa kisima cha maji katika shehia ya Kilindi Wilaya ya Chake Chake Pemba, ikiwa ni shamra shamra za miaka 51 ya Mpinduzi ya zanzibar


Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Mhe Hanuna Ibrahim Massoud, akizungumza na Wanannchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Kisima cha Maji Safi na Salama katika Kijiji cha kilindi Wilaya ya Chake Chake,ikiwa ni maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzindua Miradi mbalimbali ya Maendeleo kisiwani humo, mara baada ya kufunguliwa kwa kisima chao cha maji.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar tawi la Pemba, Mhe Juma Ali Othaman, akitoa taarifa ya kitaalamu katika uzinduzi wa mradi wa maji shehia ya kilindi Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.