Na Mwanajuma Mmanga
Katibu wa Mufti wa Zanzibar,
Sheikh Fadhil Soraga, amewataka maimamu, walimu wa madrasa na viongozi wa dini,
kutumia fursa wanazozipata kuhubiri upendo, mshikamano na utulivu hasa katika
kipindi hiki cha kuadhimisha kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW).
Alisema Mtume SAW alikuwa
muhubiri mkubwa wa amani na utulivu katika jamii.
Wito huo aliutoa jana wakati
akizungumza ofisini kwake Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Pia aliwasihi wanasiasa na kujiepusha na vitendo vyote
vinavyosababisha uvunjifu wa amani hasa katika kipindi cha uchaguzi na kura ya
maoni kuhusu katiba inayopendekezwa.
Alisema neema za amani na
utulivu ni lazima zilindwe na ni wajibu wa kila mmoja kuzienzi na kuzitunza ili
zisipotee.
Aidha aliwanasihi Waislamu
kuzitumia vyema neema anazopewa na Mwenyezi Mungu.
No comments:
Post a Comment