Na Fatuma Kitima,DAR ES SALAAM
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imetenga kiasi cha shilingi bilioni 293 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa,
uandikishwaji wapiga kura pamoja na
upigaji kura nchi nzima.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar
es Salaam na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji
mstaafu, Damian Lubuva, wakati
akitoa tathmini ya utekelezaji wa zoezi la majaribio la uboreshaji wa daftari
la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa mpya wa Biometric Voters
Registration (BVR).
Alisema zoezi hilo la majaribio limekamika katika kata za
Bunju na Mbweni katika jimbo la Kawe, manispaa ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam, kata za Ifakara,Kakingiuka,Ipangala na viwanja sitini katika jimbo la Kilombero,mkoani
Morogoro,pamoja na kata za Ikuba,Usevya na Kibaoni jimbo la Katavi halmashauri
ya wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Alisema jumla ya BVR kits 250
zilitumika katika uboreshaji huo kwa mgao wa halmashauri ya Kilombero BVR kits
80,halmashauri ya wilaya ya Mlele BVR kits 80,pamoja na halmashauri ya
Kinondoni BVR kits 90,ambapo vituo vyote vilifunguliwa kuanzia saa 2.00 asubuhi
na kufungwa saa 12.00 jioni.
Alisema koa wa Dar es Salaam,
kata za Bunju wapiga kura 15,123 waliandikishwa kati ya 27,148 kata ya Mbweni
wapiga kura 6,200 waliandikishwa kati ya 8,278 ambapo takwimu hizo zilikisiwa mapema
kutokana na matokeo ya sensa mwaka 2012.
Aidha alisema mkoa wa Morogoro
kata za Ifakara,Kakingiuka,Ipangala ,Mlabani na Viwanja sitini wapiga kura walioandikishwa ni 19,188 ambapo
ilikadiriwa kuandikishwa wapiga kura 17,790
na mkoa wa Katavi halmashauri ya Mlele kata za Ikuba,Usevyana Kibaoni
wapiga kura 11,210 waliandikishwa wakati makadirio yalikuwa watu 11,394.
Pia alisema matokeo hayo
yanaridhisha kuwa vifaa vya uandikishaji vilifanya kazi vizuri na hivyo
vinaweza kutumika katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa
nchi nzima.
Hata hivyo, alisema licha ya mafanikio kuna baadhi ya changamoto
zilijitokeza katika zozezi hilo,ambapo zilitumika camera za laptop badala ya kutumia camera iliyowekwa kwa
ajili ya kupiga picha pamoja na uchukuaji wa alama za vidole ilisababisha
mfumo kusimama.
Aliongeza kuwa changamoto
nyingine ni uandikishwaji na matatizo ya watendaji wa zoezi hilo, BVR kits
kuchelewa kufikishwa katika vituo pamoja na vurugu wakati wa uandikishwaji.
No comments:
Post a Comment