Habari za Punde

Ujumbe wa Walimu kutoka Kiruna Sweden Wakiwa Makunduchi kwa ziara yao ya kutoa mafunzo kwa Wananchi wa Wadi ya Makunduchi.


Ndugu Moh'd Simba wa pili kushoto akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli 18 kwa walimu kutoka Kiruna Sweden. Sherehe ya kukabidhi baiskeli hizo ilifanyika Skuli ya Makunduchi na kuhudhuriwa na wanakijiji. Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo ni ndugu Mwita Masemo, mwenyekiti wa Kamati ya wadi za Makunduchi ambayo imeanzisha uhusiano na Manispaa ya Kiruna. Chini ya mashirikiano wanawake wa Makunduchi watafundishwa ujasiriamali, kiingereza, kompyuta na demokrasia.
 
                           Miongoni mwa wazee waliohudhuria kwenye sherehe ya kukabidhi baiskeli
Ujumbe kutoka Nchini Sweden wakiwa katika picha ya pamoja nac wenyeji wao wakiwa katika Kijiji cha Makunduchi na Walimu Wanakamati wa Wadi ya Makunduchi na wanafunzi watakaoaza mafunzo ya Ujasiriamali 

4 comments:

  1. Ahsanteni Wamakunduchi nimependa sana kwamba wazungu hao munawafundisha utamaduni wetu wa mavazi, hio safi sana wakiwa kwetu wafaidi utamaduni wa vazi la stara.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli tunastahiki tuwaponze wana wa Kae. Nadhani wamesikia maoni yetu maana wale wage I waliokuja Mara iliyopita kwa kweli hawakuvaa nguo za stara hata kidogo hata sisi wengine tukapatwa na wasiwasi isijekuwa kuna mpango Wa sirisiri Wa kupotosha maadili yetu. Mara hoi hongereni

      Delete
  2. na vipi zile ngoma za kibara pia hawakupigiwa mara hii?

    ReplyDelete
  3. walipigiwa, so that?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.